Nahitaji msaada harakwa wa kisheria!! Majanga kazini.

Sizinga

Platinum Member
Joined
Oct 30, 2007
Posts
9,374
Reaction score
6,857
Ni story ndefu kidogo lakini kwa ufupi ni kwamba bosi wangu wa mradi-Muhindi(Project Manager) kanishutumu mimi kama mwizi iliyopelekea kuninyima allowances zangu na kunipa barua ya onyo(Memo), kitu ambacho nimechukia sana ilhali sikuhusika na hicho kitu na tayari ukweli ameshaujua. Nilimwandikia barua kali ya kuanika uovu na ubabe wake anaonifanyia na anaoufanya ndani ya mradi huo,ambayo niliipeleka ofisi kuu.

Maamuzi ya ofisi kuu baada ya kuitwa huko, yamepelekea mimi kuhamishwa mradi na kwenda kwenye mradi mwingine. Kwenye ile barua niliyompa nilimpa siku 14 awe ameniomba radhi na amenilipa kiasi flani cha fedha, na iwe onyo kwake kukurupuka kuniita mi mwivi. Siku 14 zimeisha juzi na hamna kitu alichokifanya. Sasa naomba msaada wa kumpata wakili kwakuwa hii suala limeniathiri sana mimi na familia yangu, nataka nimburuze huyu ponjoro kwenye vyombo vya sheria ambako haki itaziingatiwa.
Tayari documents zangu zinazothibitisha tukio zima ninazo na zimekamilika. Naomba msaada wa kisheria nianzie wapi au mwenye mtu wa kumfahamu wakili yooyote aniambie nikamuone kwa maelezo ya kina. Kwa sasa nipo hapa daslam.

My Regards.
 
Kwa hiyo unataka umpeleke mahakamani ukalipwe hizo allowances ambazo hukulipwa au unataka akulipe hela kwa sababu in one way or the other..umekua affected na familia yako? Unajua huko mahakamani utaulizwa umekua affected kivipi..!!
 
wasiliana na m&lamtane advocates pale city funiture darajan kama unaenda kariakoo sim 0713602026
 
Nenda ofisi za Commission of Mediation and Arbitration (CMA) zilizo karibu watakupa form ya kujaza malalamiko yako ambayo kwa upande wangu kama HR naona zaidi ni 'harrassment' ambayo ime-form discrimination na ni kinyume na Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 5, 6 na 7.
 
Hizi ndio hatua za kuchukua kaka, na kumbuka sheria za kazi zinamlinda sana mfanyakazi, ka utaweza dhibitisha madai yako basi utapata stahiki zako pamoja na gharama za kesi.
All the best :wave:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…