Nahitaji msaada kwa wenye utaalam na biashara za madini

JANIBICHI

Member
Joined
Oct 9, 2013
Posts
6
Reaction score
0
habari zenu wana JF, naamini mko vizuri na mnachakalika kikamilifu kuhakikisha mkono unaenda kinywani na kuhifadhi cha baadae.
naomba kusaidiwa na wenye uzoefu/uelewa wa biashara za vitalu vya madini, iwe ni kwa mikataba ya kupangisha au kuchimba na kugawana pato au kuuza kabisa kitalu. nikipata msaada nitajua nifanye option ipi.
kwa ufupi ni kwamba nina plot yenye ukubwa wa 6.9Ha, ipo maeneo ya SAMBARU huko Singida (kwa wanaofahamu hili eneo wanaweza wakalielezea zaidi juu ya upatikanaji wa madini) ambapo yana patikana madini aina ya Dhahabu.
sasa nahitaji mtu/kampuni mwenye akili timamu ninaye weza kuingia naye mkataba wa kuvuna hayo madini, yeye apate na mimi ni pate lengo ni kuuaga umasikini.
nahitaji msaada kutoka kwenu wana jamvi hili, ni option ipi nzuri kuifanya 1. kuuza plot. 2.kukodisha mtu/kampuni. 3.kuingia mkataba wa kuchimba na kugawana pasu kwa pasu. nisaidieni ili nisijeingia mkataba kama wakina KINJEKITILE NGWALE,
pia nakalibisha kama kunawatu hapahapa jamvini wamewahi kufanya biashara hii na wanataka nifanye nao ili tuuage umasikini basi wanieleze uzoefu wao tunaweza kuingia deal.
naamini tupo hapa kuelimishana na kuhakikisha tunamng'oa huyu adui umasikini basi dili hili hapa, usibane kama unafahamu, tiririka mwana JF.
 
Jamani hii kweli ni hatari, na ninadhani ni dalili ya kwamba hatuna wajasiliamali wanaoweza kuongoza biashara ya Madini na vitalu vya gesi ya mtwara ambao ni wazawa wa nchi hii.
bado siamini kama hakuna hata mwana jamvi mmoja alie na msaada juu ya ombi langu ijapokuwa post imetazamwa na watu wasiopungua 87.
jamani tuacheni ubinafsi kama unajua jambo basi tiririka umkomboe Mtz mwenzako. kama tutaendelea kubana namna hii basi hamna kutoka.
bado nategemea msaada wa mawazo kutoka kwenu jamani ili nifanye dili yenye kueleweka, sitaki habari ya "majuto ni mjukuu", "penye miti hakuna wajenzi" ooh mara "ng'ombe wa maskini hazai". sasa mimi napambana na ule msemo wa "mficha ..... hazai", sasa mimi nataka kuzaa jamani wacha tu nishike chupi kama bendera.
 
mkuu nimeona uzi Wako.eneo lako limefanyiwa geo -survey?una leseni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…