jerrybigbwoy
Member
- Jun 14, 2015
- 7
- 0
habari zenu ndugu zanguni nyote, mimi mpya humu na naomba yeyote awe na uhuru wa kuchangia kwa lengo la kunisaidia mwenzenu.
Jamani mimi nasumbuliwa na ugonjwa wa miguu kuvimba na kupata maumivu makali mara kwa mara maeneo ya juu ya kisigino (ankle), mara nyingine mpaka kwenye magoti na nyonga. Tatizo hili lilinianza tangu nikiwa shuleni sekondari form 3 Mbeya 2009, kusema ukweli wa mungu tatizo hili lilianza lenyewe pasipo kupata mteuko, kuvunjika wala accident yeyote.
Jamani, tangu nianze kwenda hospitali nimetumia gharama nyingi pasipo kufanikiwa, zikiwemo kuvishwa clip bandage zaidi ya mara tatu kwa kuamini ushauri wa kila daktari. Mwaka huo huo 2009, zilichukuliwa picha za mionzi (x-rays) zisizohesabika, na vidonge vya calcium orijino ambavyo kidonge kimoja kinauzwa tsh 900. Naandikiwa vidonge 60 ambavyo vinatengeneza sh 54,000, navinunua kila ninapozidiwa hasa kipindi cha baridi.
Nimetembea hospitali kibao ikiwemo Aga Khan na Hospitali kubwa ya Wahindi TMJ Mikocheni lakini sijaona ikirudi kwenye hali yake bali ni kuandikiwa dawa na kuambiwa nirudi nitakapomaliza dozi. Cha kushangaza madaktari wengine wanashangaa kuona bado nasumbuliwa.
Kuna kipindi huwa naipa sana tabu familia yangu kutokana na tatizo hili, pia limekua changamoto kubwa mno katika kufikia malengo yangu kwani ninapozidiwa tu, huwa siwezi kusimama kabisa.
Kama mazoezi huwa nafanya tena kwa kiwango chake, lakini nashindwa hata la kusema.
Tafadhalini, naombeni msaada kwa mwenye ushauri my dear na Watanzania wote naombeni mtazamo wenu please.