Nahitaji msaada wa kisheria na kielimu ili niweze kufikia ndoto zangu

Nahitaji msaada wa kisheria na kielimu ili niweze kufikia ndoto zangu

scientificall

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2015
Posts
457
Reaction score
328
Heri ya mwaka mpya wanajamvi.
Nahitaji msaada wa kisheria na kielimu ili niweze kufikia ndoto zangu.
Mimi ni mwanafunzi wa kitivo cha elimu chuo kikuu SAUT mwanza compus. Nikisoma Bacheral of Arts With Education. BAED.

Nilichagua corse kwa msukumo wa uchumi mdogo kwani mimi ndoto zangu ilikuwa nisome sheria, lakini katika mwaka wetu wa kuomba mkopo sheria ilikuwa non priority hivyo kulingana na uchumi wa wazazi wangu wakanshauri nichukue education.

Sasa juzi ndugu yangu mmoja kanipigia simu akijua mimi nasoma sheria akiniambia kuna nafasi in private company nae akiwa meneja wanahitaji mwanasheria. Iliniuma sana baada ya kumwambia nilibadilisha mawazo na kusoma education.

Mwaka huu namaliza masomo na form six nlisoma HGL je naweza soma masters ya sheria. Yaani niunge nkimaliza degree? Naombeni ushauri wenu wanajamvi.
 
Kama utahtaji ku-practice itakuhitaji usome bachelor ya sheria kabisa! Then upite lawschool.
 
Back
Top Bottom