Nahitaji msaada wa kisheria wapendwa

bujaganoni

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
561
Reaction score
453
Habari wana jamvi...!

Ninaomba nitoe story fupi kisha mnipe msaada wa kisheria.

Kuna mdogo wangu alimpa mimba mwanafunzi wa kidato cha tano mwaka 2016. Lakini mwanafunzi huyo alimaliza darasa la saba mwaka 2008 na form four 2012. Baada ya hapo hakufaulu form four. Alienda kurudia tena kidato cha tatu 2014 akamaliza 2015 na penyew hakufaulu sawa sawa, ndipo akaenda private form five 2015.
Mwaka 2015 mtihani wa Mock wa hiyo shule alipata 0 na akashindwa kuendelea naasomo kulingana na taratibu za shule hiyo. Sasa mdogo wangu akakutana naye mtaani mwaka 2016 ambapo alikuwa ajiunge form six. Akawa kampa mimba. Sasa hivi wamekorofishana na msichana anamtishia kumpeleka mahakamani kwa kuwa alimtia mimba akiwa mwanafunzi. Kisheria imekaaje hapa?

Amepewa mimba akiwa na 22 years... na sasa ana 24 yrs... tafadhali naombeni msaada.
 
Jinai haifutiki. Kama alikuwa amefukuzwa shule na ushahidi unao usio na shaka, basi hilo utamshinda. Maana wakati wa kumpa mimba hakuwa mwanafunzi na bahati nziri umri ni above 18 yrs
 
Jinai haifutiki. Kama alikuwa amefukuzwa shule na ushahidi unao usio na shaka, basi hilo utamshinda. Maana wakati wa kumpa mimba hakuwa mwanafunzi na bahati nziri umri ni above 18 yrs

Kufukuzwa shule hakufukuzwa, maana sheria zao angerudia tena form 5 kama angetaka, lkn aliacha shule ndio akakutana na huyo mdogo wangu, na haikuchukua muda mrefu, form 5 kamaliza April 2016 na wao wamekutana June 2016 na July akawa kapata Mimba. Wakati huo inasemekana alikuwa anajiandaa kwenda form six, sasa haijulikani angeendelea vipi form six wakat results zilikuwa mbovu, maybe alitaka kufanya kama Private Candidate
 
Jamaa anadai Jinai haifutiki ndio sijamwelewa vizur...
Kwa nin hakuna kesi mkuu
Hakuna jinai kwa sababu :
Kama wakifungua charge ya rape, watashindwa kuthibitisha elements za rape, haswa kuhusu ridhaa ya mhusika (consent), mwanamke wa 23 makes decisions!

Hakuna kesi, kwakuwa ushahidi wa rape is no longer practicable kwa situation iliyofikia! Hapo ajiandae kufunguliwa kesi ya matunzo ya mtoto!
 
Vipi kuhusu kidai mwanamke alikuwa mwanafunzi wakati anapigwa mimba?
Akisema alikuwa anaendelea na form six japo reality alifeli, vipi hapo mkuu
 
Wewe ni mwanasheria ama mwanafunzi wa sheria??. Nani kakwambia charge sheet itakuwa ni rape/ravish??. Mdogo wangu ukipata mteja (Client) huwa kuna vitu 4 vya muhimu kujiuliza kwanza
1. Applicable Law (kutokana na maelezo ya mteja)
2. Court jurisdiction (wapi pa kupeleka kesi husika)
3. Locus standi
4. Accrue of action / Cause of action.

Kwa maelezo ya huyo jamaa hyo option ya rape umetoa wapi?? Na kwa nini umechangua applicable law kuwa penal code section 130 and 131??
 
Umekuja kusahihisha lakini cha ajabu umeongea utumbo kuliko uliyemsahihisha.
 
Umekuja kusahihisha lakini cha ajabu umeongea utumbo kuliko uliyemsahihisha.
Wee hujatoa postion umeleta kifaa pekee/povu hata Jaji aki_dissent na wenzie huwa anatoa opinion yake bt wee ume dissent with NO REASON save for Lamentations.

Tumia Asprin 2x3 od 5/7 ikishindikana hyo dose tumia I.V Ceftriaxone 2g od 5/7 utapona povu.
 
Naomba nikujibu kwa ustaarabu!
Kesi ya kumpa mwanafunzi mimba obvious hufunguliwa kama RAPE kwa mantiki kuwa victim hana self consent, ndio maana wengi wakitembea na wanafunzi (wakathibitika) hufungwa 30 years!

Hakuna jinai nyingine hapo! Hizo ulizoweka hapo ni case analysis, ambazo hazina msaada kwa mleta mada ambaye ni Layperson!!
 
Well, ili uweze kulitatua tatizo hili hasa kwa wanasheria wenzangu hapo juu kama mlivyokua mnabishana, mnapaswa kwanza kujua ukomo wa uanafunzi ni upi, sheria gani inayohusika na matatizo ya kimahusiano na ndoa kwa wanafunzi,,, pili nakataa kabisa maoni ya mwanasheria mmoja hapo juu aliesema kua hii ni kesi ya ubakaji, hapana sio kweli, japo moja ya counts inaweza kua hio statutory rape, lakini maswalq haya tayari yameshazungumziwa kwenye sheria yake specific kabisaa.

Nikirejea kesi ya jamhuri dhidi ya emmanuel. Cleophance ya 2017 unreported, mahakama ilisema ukomo wa uanafunzi ufika pale siku ya mwisho ya matokeo ya necta taifa yakitoka bila kujali mtu uyo ataendelea au lah, na uanafunzi unatambulika pale mtu uyo anaposajiliwa rasmi ktk shule husika.... Ndugu mwenye kesi, je uyo dada aliepewa mimba huo mwaka alikua amesajiliwa na shule husika? Alisajiliwa vp kuendelea na form 5 wakat hakua na sifa zozote za kusoma kidato icho? Basi ni wazi hakua mwanafunzi kisheria, na hili naliweka wazi kua serikali chini ya wizara ya elimu haitambui form 5 ya mtu anaesoma huku ana risit, ivyo basi nafunga hesabu yangu kwamba hakukua na kosa lolote mbele ya macho ya sheria wakati wa mahusiano yao watu hao, lakini pia wote wanaonekana kua na above 20's so hata statutory rape haipo hapo.... Sheria ya elimu namba 353 ndio inayohusika na kesi hii.

Hakuna kesi yoyote hapo.
 
Hufunguliwa kama rape coz mostly victims huwa under 18 yrs ambapo kwa mazingira hayo hiari (consent) huwa sio ingredient tena. Na pia charge sheet inakuwa na 2 counts (i) Rape (ii) impregnating a school girl na kila count ina adhabu yake. Soma the education Act cap 353 na marekebisho yake pamoja na SOSPA 4/1998 utaona utofauti wa under 18 & above 18 while are students. Otherwise km ingredient ni student ili ku_constitute rape basi hata college na university ingekuwa rape. The latter wamekuwa exempted coz ya presumption of maturity.

(For more on these search MP's debate in Hansard on 23 April, 1998). Ambapo BUNGE lilitaka kupisha sheria ya kunyongwa ukibainika umebaka)

Lakin Mbunge 1 akasema nanukuu

"Hamad Ali Musa (CUF) – “The death penalty for rape (as originally proposed) is too harsh. God did not send us to kill each other but sent us to multiply”.
 
The qn is which law will Apply
1. If is Sospa/penal code?? (Rape)
2. If is Education Act??? (No rape)

Sasa wewe kwa uelewa wako wa sheria kwa mazingira aliyosema "MTEJA" utatumia sheria ipi??

Amini amini tatzo kubwa ninalotokea kwa wanasheria uspokuwa makini ni sheria ipo kutumia kwa mazingira/facts uliyopewa na mteja.

Na pia kumbuka "WRONG CITATION OF LAW OR SECTION vitiates the proceedings.
 

Attachments

  • The+education+Act.JPG
    64.1 KB · Views: 46
Zunguka kwote mkuu ulieleta hii post, lkn shortcut jibu lako utalipata hapa.
 
Sheria Na. 4/2016 iliyorekebisha sheria ya Elimu sura Na. 353 toleo la mwaka 2002.

Imesainiwa na Mhe. John Pombe Magufuli mnamo tarehe 07/07/2016 kuwa sheria kamili.

Nakuomba ukasome "DEFINITION SECTION" ya sheria mama yenyewe ili ujue tafasri ya maneno hayo.
 

Attachments

  • Act+No.+4+of+2016.png
    400.7 KB · Views: 42
Sheria Na. 4/2016 iliyorekebisha sheria ya Elimu sura Na. 353 toleo la mwaka 2002.

Imesainiwa na Mhe. John Pombe Magufuli mnamo tarehe 07/07/2016 kuwa sheria kamili.

Nakuomba ukasome "DEFINITION SECTION" ya sheria mama yenyewe ili ujue tafasri ya maneno hayo.
 
 

Attachments

  • Act+No.+4+of+2016.png
    400.7 KB · Views: 44
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…