Nahitaji msaada wa mawazo juu ya biashara ya mifugo (ngombe & mbuzi)

Wajiokotee kidogo (uoto uliosalama).
Wapatie suppliments (za kununua).

Kikubwa kinachopatikana kuwaachia wazurure ni wao kuweza kula kwa wakati na kiasi wanachohitaji.
Ng'ombe wa kufugwa bandani wanalazimishwa kula kila wanapolia, lakini ikumbukwe sio milio yote ni njaa. Akivimbiwa uzalishaji ni mdogo sana.

Kingine anayezurura anapata mazoezi, yanasaidia mmengenyo wa chakula. Ikumbukwe Ngombe hucheua na kutafuna tena. Huyu wa kufungwa uwezo wake wa kucheua ni mdogo kulinganisha na mzururaji kwenye padoki.
 
Mkuu binafsi naona inawezekana japo yaweza kua gharama maana anaweza kutumia
1. Rotational grazing ambapo ataweka kitu kama padock /cage /kizuizi ng'mbe wanachunga eneo la ekari kadhaa huku eneo jingine limefungwa ng'mbe awawezi kucross kwenda upande mwingine then pale upande mmoja umepungua malisho unafungulia upande mwingine mzunguko unaenda hivo kule wakimaliza huku pia panakua tayari malisho yameshakua kutumika.

2.Established pasture hii njia anaweza kua anapanda majani yake mwenyewe kama chloris gayana ,cenchrias ceriaris na n.k so itasaidia kuhakikisha uwepo wa malisho ya kutosha kwenye maeneo yake.

3.Kustore malisho kama kutengeneza hay na silage ni njia moja wapo bora ya kutunza malisho.

4.kutumia mabaki ya mazao mfano utakuta kwenye eneo lake kuna wakulima wa mahindi baada mavuno anaenda kuomba mabua anayakusanya kwa wingi anapereka shambani kwake yanachanganywa na molases kuongeza ladha ng'mbe wanatumia.

5.kutumia concentrates zenye mashudu ya pamba au alizeti,pumba ,madini nk
 
Daaah mkuu unajitoa sana katika kuelimisha, unapatikana wapi?
 
Kwa upande wa Artificial insemination tz bado atujaanza kuvuna mbegu kwa madume wa ng'mbe asilia AI inatumika zaidi kwa ng'mbe wa kisasa kama frisiean na arshire only pale naic arusha wanafanya hio.
Ila pia hio ni expensive kumlipa mtaalamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…