Nilitumia dawa za Malaria aina ya Co-Malafin,nilitumia siku tatu,baada ya hapo,siwezi kukaa juani au sehemu yoyote ile yenye joto!yaani Mwili unachomachoma mpaka vinatokea vipele na vinauma sana,sasa inabidi nitafute baridi au maji nijipakepake au kivuli,nikishafanya hivyo mwili unarudi ktk hali yake ya kawaida na vipele vinapotea,sasa niliamua kurudi hospitali wakanambia ni sumu ya hizo dawa!basi wakanipa dawa za kutoa hiyo,lakini bado,nikarudi tena wakanipa dawa zingine nikatumia lakini wapi,nikarudi kupima damu wakakuta kuna malaria na typhoid nikapewa dawa na ikabidi niombe sindano sababu nimekunywa dawa mpaka nkapata vidonda tumboni,dr akaniandikia sindano,za malaria na Allerge nikamaliza lakini hakuna mabadiliko yoyote!yaani kutoka nje mimi usiku au asubuhi sana kabla ya jua,napata shida sana!nashindwa fanya kazi sababu joto na mimi ni sawa na paka na panya,yaani mimi na kivuli, kivuli na mimi!hata ktk daladala siwezi panda ka watu wamejaa!inabidi nipate siti yenye dirisha ili niliache wazi!sasa naombeni msaada wenu ili niweze pona!naamini ntapata ufumbuzi toka kwenu!nahitaji sn msaada wenu! by Calcia.