Nahitaji mtoto wangu tu, sheria ikoje

Nahitaji mtoto wangu tu, sheria ikoje

kipusy

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
639
Reaction score
323
Nimegundua mke wangu anatoka nje miez sita sasa kwa ushahidi wa kuwarecord kwa kutegesha recording kwenye simu yake baada ya kuchoka vitimbwi na kutopewa haki ya ndoa mara kwa mara na kuchelewa kurudi home pia safari nyingi kila weekend. Nikaamua kumtenga chumba baada ya kugombana na pia kutopata msaada kutoka kwa ndugu na wazazi wake kwani cku zote wamekua wako upande wake hata afanye baya gani.

Baada ya kumtenga chumba akaanza kushughulikia uhamisho kwan yeye ni mwalimu wa primary. Nilimihamishia mkoa ninao fanya kazi mimi cha ajabu halmashauri ya jiji imempa uhamisho, na mtoto wangu kamtorosha(ana miaka 6) na kwenda kumuanzisha darasa la kwanza mkoa mwingine wakati tayari nilishamtafutia shule nzuri english medium. Naombeni msaada wa mawazo na SHERIA.
 
Lakin still bado cjampa taraka, je anahaki ya kumficha mtoto nisipopajua???
 
Hapa naona hamna madesa, bado tunasoma school of law.....
 
Mtoto atakuwa chini ya mama yake mpaka atimize miaka 18 au ithibitishe kuwa mama hana uwezo wa kumlea. Ila wewe unable haki ya kumwomba mtoto wako pia ni wajibu wenu wazazi kuhakikisha mtoto anapata mahitaji yake yote mhm. Tafuta sheria ya mtoto ya mwaka 2009 hata ukigoogle inapatikana.
 
Idunga hizo sababu nazikubali kama ukiangalia post yangu nimeandika kuwa ithibitishwe kuwa mama hawezi kumlea. Ila hilo la umri kwa sasa Kuna mabadiliko Kuna decision tayari zimeisha tolewa pia sheria ya mtoto inatafsriri mtoto ni nani. Pitia sheria na maamuzi ya mahakama.
 
mkuu, mtoto anatakiwa kukaa na mama hadi atimize miaka 7, sio 18, na hiyo saba ikiisha baba ndio anao uwezo kufanya application ili aishi na huyo mtoto, kuna mambo mengi yatazingatiwa ili baba apewe mtoto, cha kwanza ni maslahi bora ya mtoto (best interest of the child), na nyingine ni mawazo ya mtoto mwenyewe anataka kukaa na nani na kama akilazimishwa kukaa na baba itamuathiri au la. hata hivyo, mtoto anaweza kuishi na baba hata kabla ya miaka 7 haijaisha kama kutakuwa na sababu ya msingi kuonyesha kuwa kukaa kwake na mama kutamuathiri mtoto; mfano, mama amekuwa chizi/kichaa, mama anamnyanyasa mtoto (wazazi wengine wanawapiga watoto hadi kuwachoma moto kuwajeruhi etc), kuna mambo mengi. kwa maelezo zaidi, bofya hapa SHERIA KWA KISWAHILI

Mkuu nakubaliana na wewe kwa ulicho kisema ingawa nina standard seven of education level nilikalili,ha!ha!mchana mwema.
 
Wa kulaumiwa ni wewe uliyekuwa unatoa huduma ambazo ziko chini ya kiwango cha TBS... Sasa kapata mzalishaji wa bidhaa bora ndio kaamua a switch to another producer... Cha muhimu hapo, kama kweli umeamua ku give up, kisheria huna haki ya kumchukua mtoto mpaka atimize miaka saba. Pia una haki kisheria na kikanisa (iwapo wewe ni Mkristo) kuvunja ndoa kwa grounds za kwamba mwenzi wako hakuwa muaminifu kwako. Then tafuta mke mwingine uoe na maisha yako yaendelee.
 
Back
Top Bottom