Acheni kugeneralise mambo. Kwani watu wangapi wenye Toyota wanaenda kutengeneza magari yao kwa mawakala wa Toyota Tz?? Wanagapi wana huo ubavu?? Au wangapi wananunua spare original za Toyota au kwa mawakala rasmi wa Toyota hapa nchini?? Tukisema na wa landrover aende CMC basi na wenye Toyota waende Toyota tanzania, wa suzuki waende CFAO n.k
Kwa nini iwe kitu cha ajabu kwa mtu mwenye gari tofauti na toyota kuulizia spare au mafundi kwenye forums?! Mbona wa toyota wakiulizia spare au mafundi hatuoni hizi comments za kubeza watu.?!!
Mtu ameomba msaada wa spare au fundi mnaanza kubeza choice yake, nadhani si uungwana, sioni logic. Mbona amepata sasa bila kwenda CMC?!!
Yes kuna magari kuyamantain ni ghali zaidi ya mengine ila bado sioni haja ya kumbeza mtu anapoulizia options za kuminimize maintenance costs.