Nahitaji mtu muhimu "potencial man" kwaajili ya kushirikiana naye kibiashara

Daud Johnson

Member
Joined
Apr 9, 2018
Posts
41
Reaction score
14
Habari zenu wakuu, mimi ni kijana mtafutaji, naishi Dar maeneo ya chanika.
Kitaaluma ni mwanasheria ila kwa sasa nafanya biashara katika ofisi yangu binafsi.

Lengo la mimi kuja kwenu ninahitaji mtu ambaye yupo tayari kushirikiana nami katika biashara yangu yaani tutengeneze partnership kwaajili ya kupata kipato.

Biashara ninayofanya inahusiana na vifaa vya ujenzi, na ninaifanyia katika eneo la kwangu mwenyewe ila changamoto niliyonayo ni ya mtaji.

Kwakweli nimepiga hatua ya kutoa huduma tofauti na kipindi cha nyuma japo sio kubwa sana na nimeishafanya utafiti na kugunduwa mahitaji ni makubwa sana ikiwa ni pamoja na watu kuja ofisini kwangu na kuniulizia mahitaji mbali mbali ambayo sina kutokana na upungufu wa mtaji.

Hivyo naomba yoyote atakayekuwa tayari kushirikiana nami anitafute. Mawasiliano yangu ni 0719913828. Asanteni

 
Sasa lawyer mzima kama unaandika potencial badala ya potential tukueleweje sasa, pia na sheria yako umeshimdwa angalau kueleza kinaga ubaga inahitajika mtaji kiasi gani ukaona picha yako inatosha kuelzea unachotaka kwetu..! Ebu kuwa serious Mr. Lawyer, vinginevyo watakuelewa mnaolingana akili.
 

bigmind mbona unakuwa na small mind

Kama uko interested mfate pm au mcheck kwa namba zake za simu katoa

Hayo mambo mengine ya kukosea achana nayo ushajua kakosea wee mwerevu mwachie mwenyewe
 
Ni Law sio Linguistic
 

Tatizo una uwezo mkubwa wa kukariri kuliko kuelewa! Hivyo nakushauri uongeze bidii ya uelewa wako. Kama ujumbe haujauelwa ujuwe si wa class yako bro.
 

Start small, I dont believe in Public request for partnership
 
Partnership kibongo bongo mizunguo sana, tumejengwa kwatika misingi ya ubinafsi, tamaa, usaliti na uvivu. Idea yako nzuri lakini jaribu kutafuta namna nyingine ya kuongeza kipato chako au kukuza capital yako ili uweze kufikia malengo uliyojipangia. Partnership atakuzingua tu na kukurudisha nyuma, wabongo hatujafundishwa kuhusu mambo ya ushirikiano katika Investment.
 

Ni kweli kabisa bro, pia nimewahi kusikia changamoto kama hizo, ila sitaki kuamini kuwa haiwezekani kabisa kumpata mtu sahihi katika hili
 
Ukiona mtu anataka kukupa fursa basi juwa kwamba wewe ndiyo fursa yake
 
You may be right bro, and I'm struggling enough to make sure things comes better, but still there's a big gap between my capital and the demands. That's why I'm here bro.

start small, I am insisting.... even go and borrow cement in a big store and pay when you sell, but getting a partner and be a part of your business will destroy your dreams, I am speaking from experience!
 
start small, I am insisting.... even go and borrow cement in a big store and pay when you sell, but getting a partner and be a part of your business will destroy your dreams, I am speaking from experience!

Thanks for the advise bro.
 
start small, I am insisting.... even go and borrow cement in a big store and pay when you sell, but getting a partner and be a part of your business will destroy your dreams, I am speaking from experience!
Great advice
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…