Nahitaji Mwanamke umri 22-28

MtamuMix

Senior Member
Joined
Feb 10, 2018
Posts
119
Reaction score
138
Mwanzo 2:18
Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Mwanamke aliye na vigezo vifuatavyo, kama uko tayari karibu PM zote zitajibiwa
1. Uvaaji, anayejiheshimu
2. Urembo- anayependa kuwa natural. Wewe kama kope bandia, rangi bandia, nywele bandia, maziwa mpaka uyaboost, hips bandia kila kitu bandia, usipoteze muda wako.
3. Mwanamke anayejitambua potentials zake. Hivi unajua mwanamke ana nguvu nyingi sana na ana uwezo wa kukufanyia chochote na usifurukute. Wanawake wengi siku hizi hawajitambui ndo maana wanalalamika tuu. Jifunze kisa cha Esta katika biblia. Aliingia kwa mfalme bila kubeba vipodozi lakini alishinda. Alipoolewa na mfalme aliushikilia moyo wa mfalme chochote alichotaka alitimiziwa ila kwa hekima ya ajabu sana (jifunze jinsi alivyomchomea Hamani mpaka mfalme akatangaza auawe Hamani).
4. Elimu kuanzia kidato cha nne hadi degree ya kwanza.
5. Body shape: Mguu wa bia, kifuani nako uwe umejaliwa, sipendi flat screen.
6. Rangi: Kuanzia weusi, maji ya kundena mweupe. Weupe kama ule wa kujipodoa (hata kama ule wa asili) hautakiwi.
7. Dini: Yeyote
8. Awe na ukomavu wa kiakili kuhusu maisha. Awe na ubunifu wa maisha na mchakarikaji.
9. Urefu. Size ya kawaida (Mrefu sana na mfupi sana hawatakiwi).
10. Mahusiano- Kuhusu mahusiano kufikia hatua ya ndoa itategemea kama utafuzu katika mizaia yangu.
 
Nimependa sana vya vigezo hivi mkuu. Hii mambo ya kupiga jeki matiti na kujikoboa mpaka uwe kama papai sio wala nini. All the best kwenye utafutaji. Naamini wapo wasichana wazuri sana hapa wanaofaa kuwa mama wa watoto wetu wanaume tunaojielewa.
Mungu akutangulie sana katika safari hii
 

Hahahaaaaaa, iko kazi. Hii screening itakuwa baab kubwa. Ila siku ya kwanza inapita no candidate. May be vigezo havitekelezeki
 
Dah vigezo vichache hapo vimeniangusha, anyway kila rakheri Mkuu, upate hitaji la moyo wakoo
 
Kwa vigezo hivyo labda umuumbe mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…