Ndugu zangu nawashukuruni sana kwa jinsi mlivyonifariji, sikutarajia hata kidogo kupata positive and constructive ideas. Mliusoma ujumbe wangu kwa makini, mkautafakari, mkauelewa, mkaingiwa na huruma na kisha mkakubali kutumia muda wenu kuniandikia kwa lengo la kunishauri, kunipa pole, kunifariji na kisha kunipa matumaini mapya na mori kwamba kwake yeye Muweza hakina kinachoshindikana panapopatikana mapenzi yake. Nawashukuruni tena kwa hayo yote. Kuna walioniandikia kwa wazi na walioniandikia kwa siri, nyote nawashukuru sana. Mawazo yenu na ushauri wenu ni hazina kubwa sana kwangu. Kwakutilia maanani umuhimu wa kila lililosemwa nanyi nimeamua kutengeneza matrix ila kila wazo lililotolewa nilizingatie katika kufanya maamuzi magumu. Kwa mujibu wa jumbe nyingi tofauti nilizopokea wazini na sirini, nimejifunza kwamba UKWELI UNALIPA kwakuwa niliyowaeleza ninyi hayakuwa jokes za net bali ni dhahiri yaliyonifika na nimejifunza kuwa ya KHERI HUENDA KIKHERIKHERI. Mmenikumbusha baadhi ya methali zisemazo MFICHA UCHI HAZAI na MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU ili mradi tu ukweli huo hauathili your personal family life, maana nisingesema kidagaubaga nisingeyapata niliyoyapata toka kwenu. Wabillah tawfiq, Mungu awabariki sana.