Nahitaji mwenza/mke wa maisha

neysta

Member
Joined
Oct 21, 2018
Posts
43
Reaction score
66
Habari wanajamvi hususani wanawake mlio singo na mnahitaji mwenza/mme wa maisha. Nami nimehamasika kuja uwanja huu kwani nimepata shuhuda kadhaa za waliofanikiwa kupata wenza humu jamvini.

Kiufupi nina kiu kubwa sana ya kupata mke kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza familia. Nishajipanga kimaisha na kisaikolojia.

Nina akili timamu na ninafahamu kuwa mwenza wa maisha anapatikana popote pale, tena nawashukuru waliotuletea platfom hii kutusaidia sisi ambao hatupati fursa hizi sehemu nyingine kwa sababu mbalimbali.

WASIFU WANGU
Jinsia; Me
Umri; Miaka 34
Kazi; Nimejiajiri pia nimeajiriwa
Elimu; Masters in Finance and Investment
Dini; Mkristo LC
Makazi; Dar Es Salaam


Mengineyo
Nina mwili wa wastani mrefu kiasi kimo futi 5 inchi 10, uzito kg 72.

Sura ya kawaida na nina bald head( uwalaza/upara)

Situmii alcoholic drinks wala sivuti sigara

Ni husband material kwa kwel, napenda sana familia, kujituma na kuwekeza ili kujiletea maendeleo


WASIFU WA NINAEMHITAJI

1. Umri awe miaka 25-30
2. Elimu angalau diploma
3. Kazi; Awe ameajiriwa/Kujiajiri. Ila hata kama hana kazi kwa sasa, nitamtafutia shughuli ya kufanya maana naamini katika kazi.
4. Dini; Napenda awe mkristo hususani dhehebu la LC, RC, Anglikana au pentecoste
5.Makazi; Dsm, au awe tayari kuja kuishi Dsm
6.kabila; napendelea zaidi wa nyanda za juu kusini maana mmi ndio napotokea.
7. Awe na umbo la wastani, kama ni mnene asiwe mnene kupita kiasi
8. Asiwe na mtoto, nataka tuanze pamoja maana nami sina mtoto
9. Asitumie kilevi chochote
10. AWE TAYARI KUPIMA AFYA

Mengineyo
Napenda mwanamke anaejitambua na anaejua wajibu wake kama mama wa familia

Napenda mwenye kiu ya maendeleo, asiwe mtu wa tamaa.

Napenda pia awe mshauri na mwenye kuona mbali kupitia ya leo(mwenye maono)


Nawakaribisha wenye nia. Karibuni


MAWASILIANO; PM YANGU IPO WAZI HADI NITAKAPOFANIKIWA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi nyanda za juu kusini ni pamoja na sisi wa Iringa eeh?, huu Ubonge sana tu ndyo shida dah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…