Nahitaji partner wa Ufugaji wa Samaki

sir maka

Member
Joined
May 14, 2020
Posts
38
Reaction score
40
Nimechimba bwawa tatu kubwa na ndogo moja maeneo ya Ruvu, nimezungushia fensi ya mabati, nyumba ya kuishi ipo na mfanyakazi tayari yupo ikiwa pamoja na miundombinu mingine iko poa mfano pampu za maji.

Nahitaji mdau mwenye nia ya dhati asapoti kwenye ununuzi wa vifaranga na tusaidiane kwenye chakula. Anayewiwa tukutane PM.
 
Tuma picha ya mabwawa tuone na ukubwa wake.
Pia uhakika wa chanzo cha maji au kama una kibali cha kuyatumia.
Ardhi ni yako na haina migogoro?
Kunafikika mwaka mzima bila shida?
 
Umekimbia?
 
Nitakuja pm unipe shule, napenda kujifunza, kama unanikaribisha pm sema amina.
Wewe umekataa kutuma tu picha za bwawa tujifunze ila unalilia upewe shule ya kupata financial support. Wabongo shida sana[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ndugu ukitaka kufanikiwa katika ufugaji wowote ule kwanza usiwe na pupa,pili usianze kuwekeza pesa nyingi.Fanya shughuli zako zinazokuingizia kipato huo ufugaji uwe kama sehemu ya kupotezea muda unapokuwa huru na majukumu mengine.
Ungeanza na bwawa moja tu na kununua vifaranga taratibu taratibu.Hakika utafanikiwa na hautapata hasara ya kukukatisha tamaa.
 
Nashukuru kwa kunipa moyo mkuu
 
Sehemu ya kupotezea muda? Ndio maana waafrika tupo nyuma kimaendeleo by 1000 nautical miles!! Unaanzisha mradi afu unaufanya sehemu ya kupotezea muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…