Kuna options 2; kwanza unaweza kumuuzia share huyo partner ili awe mmiliki wa kampuni kwa asilimia ndogo isiyozidi share zako ili mwisho wa mwaka mfaidike wote. Pili, kama na yeye ni kampuni/entity ya namna yoyote bhasi anaweza ingia mkataba wa partnership na kampuni yako kwa kutoa support yoyote ya kibiashara, e.g marketing costs, operational costs n.k au akatoa kiasi kadhaa cha pesa ili mwisho wa mwaka apate gawio la faida. ANGALIZO: kuna utofauti mkubwa kati ya 'shareholder' na 'partner'.