TUKANA UONE
JF-Expert Member
- Jan 3, 2018
- 2,345
- 6,970
Mchungaji Msigwa
Ukihitaji salamu subiri kwanza Utopolo wamkung'ute, Kolo 5 - 1 hiyo tarehe 8, tofauti na hapo utaula wa chuya!
Bado nashangazwa sana na Siasa anayoifanya mtu mzima Peter Msigwa, sababu ya yeye kuhama CHADEMA alisema ni uminywaji wa Demokrasia huku lawama kibao akimtupia aliyekuwa Mwenyekiti wa chama chake cha zamani Freeman Mbowe.
Nadhani sasa ni muda huyu jamaa akatuambia baada ya kuihama CHADEMA atakuja na mikakati gani ya kuisaidia CCM kushinda uchaguzi na kuwasaidia Watanzania kuondokana na Lindi la Umasikini kuliko kila siku kuisema CHADEMA kana kwamba alihama huko ili aiseme!
Mimi binafsi nataka anieleze ni namna gani ataisaidia CCM kutatua tatizo la AJira kwa watu wake.
Mimi binafsi nataka anieleze ni kwa namna gani ataisaidia serikali ya CCM kutatua tatizo la vijana kutekwa, kuuawa na kupotezwa na hao wanaojulikana kama "Watu wasiojulikana".
Mimi binafsi nataka kuona ni namna gani anaweza kuwasaidia wana Iringa kuondokana na kero ya muda mrefu ya ukosefu wa maji salama ya kunywa!
Mimi binafsi nataka kuona anawanadi wana Iringa kwenye chama chake kipya ili watu wengi waunganishwe kwenye Umeme!
Mimi binafsi nahitaji kuona anawapigia kelele Watanzania na wana Iringa kuhusu Barabara ambazo zimekuwa kikwazo kwao.
Yangu ni hayo tu leo.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Mchungaji Msigwa: Nitazunguka Nchi nzima kuelezea Uongo wa CHADEMA
- Kuelekea 2025 - Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM