Blauzi mbovu
Member
- Oct 30, 2021
- 39
- 35
Habari zenu wakuu !
Leo nakuja kwenu nikihitaji ufafanuzi wa masuala kadhaa yanayohusisha kodi ya biashara.
Ni kiasi cha miaka minne sasa tangu niingie ktk ulingo wa kutafuta maisha kupitia biashara.
Nimekuwa nikihangaika na biashara tofauti tofauti za kila namna lengo niingizie kipato ambacho kitaendesha maisha yangu na ya familia yangu.
Nimewahi kufanya biashara ya kuuza viatu vya mtumba mtaani, nimeuza mchele, pumba, madagaa nk.
Lakini katika mihangaiko yangu yote sijawahi kujua ni nani ktk wafanya biashara anapaswa kulipa kodi.
Nilipkuwa nikiuza viatu niliambiwa nikate kitambulisho cha mlipa kodi (20,000/-) kwa mtendaji, nikaenda nikakata, Nikifahamu sababu ya kuambiwa hivyo ni udogo wa mtaji wangu ambao ulikuwa chini ya milioni 4.
Kwa sasa nimeshaacha hiyo biashara baada ya kuona hailipi,
Nimeamua kutafuta frem na kufungua biashara ya vitu vya kupima ambayo pia mtaji wake hauvuki milioni 4.
Haikuchelewa wakaja TRA kunihoji kama nina TIN# na kama nimeshakadiriwa kodi. Nikawaambia mie huwa natumia kitambulisho cha mjasiria mali kwa kuwa mtaji wangu ni mdogo. Wakasema hapana hatuangalii mtaji, wakanambia ukifanya tu biashara kwenye "FREMU" tayari unaingia tk walipa kodi wa biashara.
Hili likanishangaza ! Lkn kwa kuwa wao ndio wataaluma wa mambo hayo nikakubaliana nao nikaenda ofisini kwao wakanikadiria kodi ambayo mpaka sasa nalipa.
Leo nakuja kwenu wanajamii forum mniondolee ule mshangao kwa kuwauliza;
Hivi ni kweli "FREMU" ya biashara ndio kipimo cha mtu kulipa kodi ya biashara ?
Pili, uelewa wangu wa kuwa ili ulipe kodi ya biashara ni lazima uwe na mtaji unaoanzia mioni 4 ? Na kama sio, basi ni kuanzia mtaji kiasi gani utalazimu mtu aingie ktk kodi ya biashara ?
Ni hayo tu ndugu zangu, niwatakie siku njema.