Inategemea na uhitaji wako/lengo la wewe kufuga, je ni kwa ajili ya:
*nyama
*mayai
*nyama na mayai
Black astro ni kuku wazuri lakini kwa ajili ya mayai kwenye nyama hawako poa
Kwa jinsi sasso walivyopatikana (evolution yao) ni wazuri katika utagaji wa mayai.
Kuroiler wao ni wazuri katika kutengeneza nyama japokuwa wote (sasso na Kuroiler) wanataga na kutengeneza nyama.
Unaweza kuwafuga kienyeji, Kuroiler na sasso na baada ya miezi mitano wataanza kutaga, kwa nyama itakuchukua wiki 10-12 kuanza kuwauza hapo watakuwa na kg Kuanzia 1.4 na kuendelea
Lakini kitu walichonacho kwa pamoja ni kutokuwa na uwezo wa kuatamia mayai unaweza kuta katika (sasso / Kuroiler) 10 ni wawili wenye uwezo wa kuatamia.
Magonjwa kuku wa kienyeji ni wavumilivu lakini kama umeamua kufuga ukifuata taratibu zote za kiafya Magonjwa hayatakuwa na sehemu kwa kuku wako, labda yale ya mlipuko.