Nahitaji ushauri please kabla ya kufanya maamuzi

ntafanyia kazi yote na mwisho wa siku ataamua yeye,kwenye kuchuja sidhani kama amekuwa matured ivo kufanya maamuzi lakini best way ni ipi kumrudisha kwao kwanza nimsaidie akiwa huko au mimi nikae nae nilee hiyo mimba maana sio kazi ndogo na mimi na watoto wadogo ndani!



 
Chauro, WOS, MTM na MBU na members wengine wametoa ushauri mzuri sana nafikiri utakuwa umepata mwanzo mzuri wapi pa kuanzia
 
Unajua hii ya kumrudisha kwao anaweza asipate uangalizi mzuri na wa kutosha halafu isitoshe sijui kama atakuwa anajua jinsi ya kujiangalia mwenyewe akiwa na hiyo mimba
 
nashukuru sana kwa ushauri wenu najua sasa nitamuuliza nini maana mengine hata hayakuwa kwenye mawazo yangu.

Chauro, WOS, MTM na MBU na members wengine wametoa ushauri mzuri sana nafikiri utakuwa umepata mwanzo mzuri wapi pa kuanzia
 
Hongera kwa moyo wa huruma na upendo ulionao
mtunze mpaka atakapojifungua
hukusema shule anasoma nini
baada ya kujifungua unaweza kumsaidia kumpeleka kujifunza
ufundi cherehani ukamnunulia na cherehani akaanza maisha ya kujitegemea
sio lazima awe fundi wa kushona chochote kile kitakachomsaidia maisha
Mungu atakuzidishia mara dufu.
 
kwa vile siku hizi wanaruhusiwa baada ya kujifungu kuendelea na masomo mi nadhani mwache alee mtoto waki akimaliza aendelee na masomo
 
Chauro una roho nzuri sana ndiyo maana ikawa vigumu kwako kukurupuka na kuamua kumrudisha huyu binti kwao mara tu baada ya kufahamu kwamba ana ujauzito. Ufahamu wako wa hali ya kimaisha kwa familia yake uliongeza huruma zako kwake maana unajua fika maisha yao ni kubahatisha kila siku iendayo kwa Mungu. Msaidie kadri uwezavyo na utapata thawabu nyingi sana. Ubarikiwe sana.
YouTube - DEBORAH COX "BEAUTIFUL U R" EXCLUSIVE VIDEO
 
Fanya number 2. Jaribu kuongea na mama yake mzazi pia kumueleza msimamo wako. Pia mtafute huyo kijana uongee naye...
 
Namba 2

Ila anaweza kuendelea kukusaidia ila duuuu I hope sio mtu usiyemtegemea

Kama anashindwa mpata simuni basi mshitue wakati yupo shule mwendee then muulize akuonyeshe na akupe full name hapo na wenzake watakuwepo

Pia ukikaa nae utajua ukweli ukimuondoa hutajua

Anaweza jua unamtumia mdogo wako kutaka kujua majibu etc

Mie wasichana wandani walichofanyia ndugu zangu siwaamini juu ya ngono wanaweza kula nawe live
 
Asante sana ntajitahidi kadri ya uwezo wang kufanya yale nayoweza.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…