Nahitaji ushauri wa biashara ya Pharmacy

Nakushauri usifungue pharmacy ila fungua duka la dawa kijijini utapiga pesa sana! Nina uzoefu na ninachokwambia!!
Nakusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Kiongozi kama hautojali naomba angalau kwa uchache saną utupe uzoefu wako...Binafsi pia niko kwenye mtanziko huo wa biashara ipi ya kufungua kati ya Duka la dawa au Pharmacy? Ningependa kusikia kutoka kwako. Asante
 
Njoo pm mkuu
 

Sorry mkuu nimechelewa kuuona huu uzi, ila najua it's never too late......

Kuanzisha pharmacy ni kazi yenye ugumu/urahisi wa wastani. Nakusaidia hatua kwa hatua japo kwa kifupi, kisha ukihitaji nikusaidie zaidi ili uokoe muda, gharama na nguvu zako utaniambia.

Hatua zake kwa haraka haraka ni kama zifuatazo:
1. Weka tayari mtaji wako (Tsh 15,000,000 - Tsh 25,000,000)
2. Tafuta eneo la kuweka duka lako (kusiwe na famasi nyingine karibu - ndani ya mita 300, fremu ukubwa square metre 30+; pasiwe karibu na dampo, sheli, kazi za moto na maeneo mengine hatarishi)
3. Ongea na mwenye eneo na upate uhakika wa kukodishiwa. Ila usilipie kwanza, mwabie utacheki naye baadae kidogo baada ya kupata confirmation kutoka kwa mafamasia wa wilaya au baraza la famasi)
4. Chap Chap Ongea na baraza la famasi au mfamasia wa wilaya ili acheki eneo lako na kukushauri kama panafaa uendelee na plan yako au hapafai na uachane napo
5. Pakiwa panafaa basi sasa endelea na plan yako na eneo hilo
6. Chap chap Tafuta mfamasia ambaye atasimamia famasi yako na ingia naye mkataba (Tsh 1,000,000 - Tsh 1,500,000 kwa mwezi). Pia pata Pharmaceutical Technicians (Tsh 600,000 - Tsh 1,000,000 kwa mwezi) na/au medicine dispensers (Tsh 300,000 - Tsh 450,000 kwa mwezi) 2 - 6 (kutegemea na ukubwa wa duka lako) ambao watakuwa wanatoa huduma katika duka lako. Ingia nao mkataba na hawa pia.
7. Chap chap lipia kodi ya fremu au eneo la watu (mara nyingi Tsh 1,800,000 - Tsh 12,000,000 kutegemea na kodi yako ya mwezi na kipindi cha miezi mingapi) kisha ukiwa pamoja na mfamasia wako anza matengenezo na maandalizi ya duka lako (Partition, shelves, taa, feni, AC, Fridge, Kabati dogo la ukutani kwa ajili ya DDA Drugs, reference materials, sinki la maji, bomba la maji, umeme, matangazo na kadhalika = Tsh 3,000,000 - Tsh 5,000,000)
8. Sasa jaza fomu ya maombi kuita mkaguzi wa eneo kutoka baraza la famasi au halmashauri ya wilaya ambako famasi yako ipo
9. Utakaguliwa na baraza la famasi au mfamasia wa wilaya, na ukikidhi vigezo basi utaruhusiwa kuanza biashara na kupewa leseni na kibali. Usipokidhi vigezo utapewa mambo ya kurekebisha kisha kuja kukaguliwa tena baada ya kufanya marekebisho. Ukikidhi vigezo basi utaruhusiwa kuanza biashara na kupewa leseni na kibali (Tsh 400,000+).
10. Nenda TRA kwa ajili ya kupata TIN na makadirio yako ya kodi (Tsh 600,000+ kwa mwaka)
11. Nenda halmashauri kwa ajili ya kupata leseni ya biashara (Tsh 250,000)
12. Nenda famasi za jumla kwa ajili ya kununua mzigo wa dawa na kuja kuuweka dukani mwako (Tsh 9,000,000+)
13. Panga dawa, fungua duka na kisha anza kutoa huduma kwa wateja wako
14. Soma movement za wateja wako, rekebisha mapungufu na endelea kujipanga ili kuboresha famasi yako
15. Tayari umefanikiwa kuanza biashara yako.

KUMBUKA MAENEO YA MSINGI:
#Plan nzuri ya famasi (Business plan, Bajeti, Mchanganuo, Strategic Plan nk)
#Vibali, leseni na kodi
#Kutii sheria na miongozo ya baraza la famasi
#Wataalam wa dawa
#Mtaji wa kuanzisha na kuendeshea biashara
#Wateja
#Marketing

Nakutakia kila la kheri na karibu kwenye biashara hii. Kama una swali au unahitaji msaada zaidi nitafurahi kukusikia tena na kukusaidia, kwani huwa naandaa na kuongoza kazi zote hizo na kumsaidia mfanyabiashara kama wewe anayetaka kufanya biashara ya dawa kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Karibu sana ...!

AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS

0788179686 | afyazaidi@gmail.com


 

kwa kuongezea tu ni kwamba Pharmacy yeyote iwe ya jumla, au rejareja, au jumla na rejareja, ni lazima iwe na mfamasia aliesajiliwa pamoja na farm technician aliesajiliwa, akikosekana hata Moja hapo hio pharmacy inafungwa haraka na balaza la pharmacy,,

mfamasia aliesajiliwa (registered pharmacist) huyu ni mtu mwenye degree ya pharmacy na malipo yao ni kati ya 700,000 hadi 1,200,000 kwa kila mwezi (huyu anafanya kaz hapo part-time au Massa 15 kwa kila wiki)

pharm technician huyu ni mtu mwenye diploma ya pharmacy na malipo yake ni kati ya 300,000 hadi 800,000 kwa kila mwezi, na anafanya kazi hapo full-time. (wakaguzi wakija muda wowote wamkute huyo pharm technician.) wasipo mkuta panafungwa.

Hawa watu wawili ndio wanaotambulika na balaza la pharmacy na kila mwaka lazima usainishane nao mkataba unao onyesha namba zao za usajili na jinsi unavyo walipa hafu pia mkataba ukasainiwe kisheria, mkataba huo lazima upelekwe balaza la famasi ili namba zao za usajili zikaingizwe kwenye mfumo wa computer, mfamasia wako atakuelekeza hapo na nizoezi la kila mwaka.

kikitokea moja wapo akahama nilazima akatoe taarifa yeye mwenyewe kwa barua hapa nilazima umpate mwingine kwa haraka ili balaza la famasi wabadili kwenye mfumo wao wa computer, vinginevyo kama hujampata unafungiwa.

vibali kutoka balaza la pharmacy kwa kila mwaka ni
pharmacy ya rejareja 200k kila mwaka
pharmacy ya jumla 500k kila mwaka
pharmacy ya jumla na rejareja ni 800k kila mwaka

Vibali vya biashara manispaa
pharmacy ya reja reja 200k kila mwaka
pharmacy ya jumla sijui wanalipaje
pharmacy ya jumla na rejareja pia sijui wanalipaje

pia kuna service levy manispaa watakuelekezea, inalipwa kila baada ya miez mitatu,

TRA
Kodi kwa pharmacy ni 600k+ kila mwaka au kama unayo mashine ya EFD unakadiliwa kulingana na turnover yako ya mwaka,, ningumu sana kuwa chini ya 600k.

Pharmacy unaruhusiwa kuuza dawa zote kwa sababu unao hao wataalam wawili niliowataja, ila duka la dwa unauza dawa baadhi tu kwa sababu hakuna wataalam wa ngazi ya juu.

Duka la dawa inahitajika cheti cha umiliki, unasoma wiki moja tu unakipata kwa kanda ya ziwa huwa wanasomea Bugando tu,, au unamtafuta mwenye nacho unatumia chake hafu unamlipa kwa kila mwezi 100k,, pia unatakiwa kua na mtu mwenye elimu ya ADO ndio anaruhusiwa kuuza dawa kwenye duka la dawa muhimu (DLDM), hapo mwanzo ADO walikua wanasomea miezi mitatu tu ila kwa siku hizi wanasoma mwaka moja, malipo kwa ADO ni 150k au zaidi kwa kila mwezi.

ukifungua duka la dawa
usiandike neno pharmacy, nikosa kubwa.

karibu kwenye biashara sis tupo Mwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…