Tafuta eneo kubwa la wazi, pata kibali manispa husika. Kuna watu wengi sana wanauza magari, au nyumba etc Kila mtu huwa anauza maliyake kwa sababu au shida alionayo mwenyewe. lakini madalali ndio wanao waangusha sana.
Katika hilo eneo la wazi kila atakae taka kuuza gari lake atalileta hapo kwako siku ya juma mosi na juma pili pekee. (Siku mbili katika wiki). Utakua unawakutanisha mnunuzi na muuzaji moja kwa moja bila dalali.
Kuhusu malipo yako weka kiingilio (5000 or 10,000) na fomu za kujaza. Kwa walio na nyumba za kuuza, watakuletea picha na bei zao. I'm sure you will end up making not less than 100,000 a day without investing more than 200,000. Badala ya watu kuweka matangazo kwenye magari "For Sale" watakua wanaleta kwako siku ya juma mosi na juma pili. Biashara hii itafaa only on weekends.
Ukiletewa gari siku ya juma mosi, owner hana haja ya kusubiria hadi jioni, anaweza kuendelea na shuguli zake na akalirudia siku ya juma pili jioni. Hapo atakuta orodha ya contacts wanaotaka kufanya nae biashara.
Advantage ya hii kazi ni kwamba muuzaji will have a better option of getting a person atakae nunua mali yake kwa bei poa.
Jinsi ya kujitangaza. Sajili jina la kampuni yako, mafano HABARI Car Auction, print brochures weka contacts zako zisambaze. Sehumu ya kusambaza hizo brochures ni wakati wa traffic lights.
Hii ni kama huna biashara unayo ifahamu kabisa.