Nahitaji vifaranga wa kuku wa nyama

Nahitaji vifaranga wa kuku wa nyama

hhsmakwato

Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
97
Reaction score
51
Habari zenu Wanajamvi,

Kiukweli nimemaliza kutengeneza banda langu kwa ajili ya mfugo wa kuku wa nyama. Kwahivyo naomba kupewa maelekezo mazuri juu ya:-

1. Kifaranga mmoja ni sh ngapi ?
2. Wapi wanapatikana viranga wazuri.Mimi nipo Tanga.
3. Ni gharama gani nitazipata kwa kila kuku kwa kipindi chote cha mfugo.

Naomba kuwasilisha
 
Hata mm nahitaji hayo Maelezo plz mwenye uelewa nayo, mi nipo DAr
 
kifaranga mmoja kwa sasa ni tsh 1300/= kwa kawaida huuzwa kuanzia vifaranga 100. Gharama ya chakula pamoja na madawa kwa mwezi mmoja uenda ikakaribia tsh 300,000. Hii inategemea na kampuni utakayokuwa unanunua chakula cha hao kuku. Kuna baadhi ya kampuni dawa nyingi wanachangahya kwenye chakula na kampuni zingine hawachanangi yaani uuzwa tofauti. Njia rahisi ya kupata vifaranga fika kwenye duka la vyakula vya mifugo lililo karibu wao wanakuwa na habari nyingi za upatikanaji wa vifaranga.
 
Habari zenu Wanajamvi,

Kiukweli nimemaliza kutengeneza banda langu kwa ajili ya mfugo wa kuku wa nyama. Kwahivyo naomba kupewa maelekezo mazuri juu ya:-

1. Kifaranga mmoja ni sh ngapi ?
2. Wapi wanapatikana viranga wazuri.Mimi nipo Tanga.
3. Ni gharama gani nitazipata kwa kila kuku kwa kipindi chote cha mfugo.

Naomba kuwasilisha

Bei ya kifranga kimoja ni TZS 1,300/-, ila kuna uhaba mkubwa ana wa vifaranga wazalishaji wengi wana shindwa kukidhi mahitaji ya soko.

Mimi hutumia kampuni ya Silver lands Ltd ya irnga wanaozalishia vifaranga vyao dar es salaam, wako vizuri kwa tanga sijui utwapataje?

Chakula chao ni ghali kidogo hivyo huwa sikitumi, natumia vyakula vya watu wengine mfuko TZS 45,000/-, Silver Lands wanauza TZS 50,000/- PER BAG
 
Mkuu sijaelewa hapo,vifaranga ni laki na 30 + laki 3 ya madawa na chakula au? = inakuwa laki 4 na 30.ndo ivo?
 
Ungetupa mchanganuo wa hao vifaranga 100 hadi wafae kuuzwa wanaeza cost shangap???
 
Back
Top Bottom