Nahitaji vijana washirika kibiashara

ChescoMatunda

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2009
Posts
1,232
Reaction score
442
NDUGU ZANGU VIJANA WENZANGU

Nimekuwa kwenye ujasiriamali kwa kipindi kirefu kidogonimepita uzoefu mwingi ikiwamo kushindwa na kuamka na kuendelea na sasa nimeonelea nishirikiane na WENZANGU uzoefu huu kwa pamoja, lakini kubwa, UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU.

Nimepata wazo la ushirika kwa vijana tuu tena ujasiriamali kwa waliotayari kutumia uwezo wao na bidii zao kufikia mafakio tuyatakayo. Unachotakiwa kufahamu ni unatakiwa uwepo kama mshirika kibiashara Yaani. (BUSINESS PARTINER)

KWENYE ujasiriamali usiohitaji uwekezaji mkubwa niseme ni Karibu na bure kwa sababu huhitaji kuwa na PESA zaidi ni efforts yako ndio kitakuwa kigezo cha kwanza na uwekezaji wako, pili uwe tayari kusimamia na kushiriki mchakato Mzima kwa ukaribu kigezo kingine nitahitaji umri usizidi ujana ili kukidhi malengo tarajiwa kibiashara tukianza vijana kumi mwanzo mzuri zaidi.

Haichagui jinsia wala dini kwa alietayari kushirikiana nami au unamfahamu kijana mwenye mawazo chanya kama yangu tuwasiliane kuanzia hapa au chescomatunda@gmail.com 0765555030.
 
Upo serious au unawazingua vijana. Mbona unafichaficha wazo la kibiashara ulilo nalo. Nadhan ungeweka wazi tulipime wazo lako hata kama ctakuwa mm naweza kuwafaham vijana unaoweza kushirikiana nao. Ucjipe mzigo wa kupokea sim kujib maswali ya m1m1. Nawaza tu.
 
Mmetutosa kimtindo kwa kutumia kigezo cha ujana, si wazee sijui twende wapi maana Tanganyika/tanzania legion nayo imebomolewa
 

Niko serious mkuu ila kama uko interest tunapanga meeting mzee sio maskhara . kuhusu kuweka hapa aina ya wazo langu la biashara sina uhakika na haki miliki ya wazo langu kwakuwa sasa vijana wengi sio wabunifu waigaji na huharibu hata image ya wazo pia. Mfano nilikuwa wa kwanza kufungua kona matunda pale Africa sana baadae unajua nini kilitokea kila mtu anataka afanye biashara hiyo hiyo.
 
Mmetutosa kimtindo kwa kutumia kigezo cha ujana, si wazee sijui twende wapi maana Tanganyika/tanzania legion nayo imebomolewa

Mkuu hujatoswa unaweza kutuunganisha na vijana wa Karibu yako utakuwa umeshiriki kwa namna hiyo pia..
 
Uko sawa mkuu ila sisi wenye 40s unatupokea au tumezidi umri
 
Mia mkuu,
nilitaka kushangaa hata jukumu la kuhamasisha tushindwe, ila toa dodoso si unajua vijana wamezoea utapeli wa siasa, Wasije kufikiria naanza kampeni za siasa mapema.
Mkuu hujatoswa unaweza kutuunganisha na vijana wa Karibu yako utakuwa umeshiriki kwa namna hiyo pia..
 
Chesco Mzee wa Matunda, kumbe ni wewe.

Swali langu ni wapi ambapo wazo ulilonalo litafanyika(Location), kumbuka forum hii wanaingia watu toka maeneo tofauti.

Kuhusu watu kutaka kufanya biashara kama yako hio ni kawaida na duniani kote inafanyika hivo ila la msingi wewe kama mjasiliamali unapaswa kuwa m-bunifu kwa kuongeza thamani/mvuto/kuboresha zaidi ili kuwa tofauti na wenzako waliokuiga.
 

Uko sahihi mkuu katika ushindani kunahitajika kuboresha kila siku ili kukidhi ubora na ushindani makini. kuhusu wazo hili sitaki kuanza na mshindani wakati mmoja vinginevyo najua kuna watakaoiga ila lengo ni kuanza na wazo binafsi ili waigaji wafuate njia, tutaanzia Dar kwa sasa afu tunapanua wigo hatua kwa hatua.
 
Well mkiwa mnapanga kupanua wigo niko tayari kuungana nanyi pia. Pamoja sana
 

Huo si ndio ushindani wenyewe boss kubwa inabidi uwe mbunifu ku survive.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…