Nahitaji wakili ambae anaweza kusimamia kesi ya mauaji

hp4510

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
7,235
Reaction score
7,392
wakuu habari za majukumu, kuna ndugu yangu amepatwa na kesi ya mauaji ila kwa mujibu wa maelezo yake anasema siku ya tukio yeye alikuwa mkoa mwingine kikazi, kwa sasa huyo ndugu yangu anashikiliwa na police naitaji msaada wa wakili ambae anaweza kudeal na kesi kama hiyo
 
.........mtafute Mheshimiwa Magafu Majura ni Expert sana.
 
.........mtafute Mheshimiwa Magafu Majura ni Expert sana.

Hata mimi nimetaka kussema mtafute magafu majura ameshasimamia kesi yangu aise usipime ndugu yule ni mtambo....kama unataka simu yake ni pm nitakuipa
 
aisee gharama zake ziko vipi ? office zake ziko wapi ? naomba msaada wa number yake
 
ndugu tukio limetokea lini?kama ni mwaka huu,bado mapema kuweka wakili,kwani kwa kawaida hadi upelelezi ukamilike,na kwa kipindi hiki,bado kesi itakuwa mahakama ya hakimu mkazi/wilaya ambayo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji na mtuhumiwa haruhusiwi kujibu chochote kisheria,sasa hapo wakili wanini?Kwa ushauri zaidi nitafute.
 
aisee gharama zake ziko vipi ? office zake ziko wapi ? naomba msaada wa number yake
Gharama zake inategemea na uzito wa kesi yenyewe kiongozi, ni Wakili maarufu sana anapatikana Dar es salaam; kwa karibu sana zungukia mitaa ya Mahakama kuu au pale Kisutu Mahakama ya Hakimu Mkazi..uliza mtu yeyote pale utajulishwa ni wapi anapatikana kiurahisi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…