Nahitaji watu watano tuunganishe ujuzi

sojer

Member
Joined
Sep 4, 2018
Posts
71
Reaction score
47
Hi JF members
Poleni na majukumu
Nimeona ni vema nikaanzisha hii ID mpya ili kusudi niwe natupia mambo nyeti ,muhimu na yenye tija kwetu sote najua sitawaridhisha wote kutokana na kila MTU kuwa na hulka yake ya vitu anavyovipenda na kuna wengine nitawaridhisha kwa kiasi chake na hatimae watakaokuwa tayari basi tutaungana!

By professional Mimi ni mwalimu !
Lakini ni mjasiriamali mdogo kiuchumi lakini mkubwa kifikra na mwenye ujuzi kadhaa nasema hivo kwa sababu miezi kadhaa nyuma nilikuwa ni mkufunzi wa masomo ya ujasiriamali katika vikundi mbalimbali huko mikoani na nilikuwa nikiyafundisha bure bila malipo japo nilikuwa na mradi wa kuuza vitabu vya ujasiriamali ambapo nilipata fursa kubwa ya kuuza vitabu hivyo kwa hao wanakikundi na hio ndo ilikuwa ridhiki yangu kwa wakati huo lakini nikaja kusimama kufanya shughuli hizo baada ya kuanzisha mradi mwingine ambao nao nilienda nao kwa kipindi Fulani na kuuacha na saivi nipo na huduma nyingine inayonipa kula kulipa pango na kutimiza mahitaji yangu

Back to the point!

Nina wazo kuu limenijia kichwani na nimelifikiria nikaona ni vema nikapata wenzangu wanne ambao wako serius na wako tayari kwa UDI na uvumba kuhakikisha kuwa kitu tutakachokianzisha hakiishii njiani yaani afe kipa ama beki ila mradi lazima usimame kwa vyovyote na kuhakikisha kuwa tutashikana mkono mpaka point ya mwisho!

Miradi niliyofikiria ni hii ifuatayo:
Mradi 1: UTENGENEZAJI WA CHAKI
Mradi 2:UTENGENEZAJI WA SABUNI YA MCHE
MRADI 3: UTENGENEZAJI WA MAFUTA YA MGANDO AMA LOTION N.K

MIRADI HII NI MIRADI AMBAYO INAWEZA KUTUFIKISHA PALE TUTAKAPOHITAJI TUFIKIE KIUCHUMI kikubwa ni kuwa serius na kazi na kizuri zaidi Nina IDEA YA ELIMU YA HIVO VITU ILA TUTAKAPO KUBALIANA BASI TUTAANZA NA MOJA NIKIWA NA MAANA YA KUTAFUTA UJUZI WA KUTOSHA,MALIGHAFI KWA GHARAMA NAFUU,SOKO NA VIBALI VYA UZALISHAJI PAMOJA NA MATANGAZO YA PRODUCT YAKO KAMA UNAJIONA UKO SERIUS NI PM AFU TUTAANZISHA GROUP LA WHATSAPP LA WATU WANNE AU WATANO TUTAKAOKUBALIANA NA KUJADILI KWA KINA ZAIDI

Narudia tena nataka watu serius tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningetaka kujua wewe upo wapi Dar au mkoani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wazo zuri mkuu,vipi kuhusu masoko ya hizo bidhaa na faida inaweza kuwa kiasi gani?na sisi tuwe na mtaji kiasi gani?
 
nimependa wazo lako,ila changamoto iliyopo nipo mkoani lakin pia tunaweza kufanya hiyo kazi;kama hutojali jaribu kufafanua ni kitu gani sisi washirika tuwe navyo
 
Ni wazo zuri sana! Wewe mwenye wazo ndo unajua kiundani hata kwa mchanganuo tu

Elezea kdg ilitujue hasa mlengwa ni mtu mwenye mtaji kiasi gani? Au ni mtu tu alie serious!
Ili tujipime......

1: Mchanganuo wa kiwango cha chini

2: kiwango cha kati

3: hata cha juu kdg!

Mi nafikiria ungeanzisha group LA whatsap ili ktk mawasiliano huko kila mtu atajipima.

Watano watapatikana na wengine ambao watabaki watapata nao wazo zuri zaidi!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu serius ndio watu wa aina gani wewe mwalimu?

Wewe ni mwalimu kweli?? serius ndio nin?

MNAKERA MNOOOOOOOO
 
Mimi niko tofauti, wazo langu napendekeza ufugaji wa kuku broila
 
Reactions: etb
Kwanza nikupongeze mkuu kwa kukaa chini kuweza kuandika hoja ambayo inaweza kutoa utata/fumbo kwa wengi

Kila jambo linaanza na majaribio kwanza ili kusudi baada ya kujaribu tutaweza kukaa chini kujadili matokeo tuliyopata na hapo ndipo tutaamua kuwa wapi turekebishe na wapi tuboreshe

Kuhusu mitaji
Kwa kawaida mitaji hii inategemeana na sisi tumejipangaje kwani tunauwezo wa kuzalisha locally(yaani bila kutumia mashine means tutatumia vitu vinavyotuzunguka)
Minimum mtaji nikama 200000
Mtaji wa kati ni kama 500k hadi 1500k
Mtaji mkubwa ambapo tutahitaji mashine na vifaa vingine ni kama milioni tatu+



Mlengwa ni MTU yeyote mwenye nia ya dhati sio yule ambaye anataka kujaribu afu atuache njiani tunataka tupanue wigo na hatimae tutaweka na branches mikoa yote tz ila mwanzo mgumu na ili kutatua hili inabidi tuanze kidogokidogo
 
Elezea niwepp
Tunakodi mabanda bunju( wazo) tunanunua vifaa vya chakula nk, tunakubaliana idadi ya vifaranga wa kuanza nao, 500-1000,Tunapiga budget ya chakula chao na dawa, tunafuga ndani ya wiki nne tunauza tunagawana faida, mtaji unarudi tena kwenye cycle.
 
Tunakodi mabanda bunju( wazo) tunanunua vifaa vya chakula nk, tunakubaliana idadi ya vifaranga wa kuanza nao, 500-1000,Tunapiga budget ya chakula chao na dawa, tunafuga ndani ya wiki nne tunauza tunagawana faida, mtaji unarudi tena kwenye cycle.
Wazo zuri,tafuta soko kwanza tuingie nao mkataba wa ununuzi baada ya miezi sita kuanzia sasa,ili tuwezekuwekeza kwa juhudi zote.kuliko kufuga halafu tuanze kutafuta soko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…