Mwendabure
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 2,138
- 1,044
Waungwana salam! Mimi ni kijana mwenye elimu ya darasa la saba nipo Dar. Napenda TEKNOHAMA (Teknolojia ya habari na mawasiliano) kiasi nimeweza kujifundisha kutumia kompyuta si haba! kwa msaada wa kibarua mwenzangu na juhudi binafsi nilifanikiwa kununua kompyuta (laptop)kuukuu ambayo inaonyesha dalili zote za kuchoka kabisa. Basi waungwana naomba mnifahamishe ni aina gani ya kompyuta itanifaa na ikiwezekana na mahali muafaka ambapo nitapata pia maelekezo na ushauri wa ziada kwa kuzingatia uchanga wangu ktk ulimwengu wa kompyuta na elimu ya kutosha ya darasani. Kwani kila ninapoenda sipati msaada ninaohitaji zaidi ya wahusika kuwaka tamaa na uchu wa fedha zangu na kutaka kunibambika 'kimeo' hasa baada ya kuwaeleza wazi kuwa sina weledi sana ktk mambo ya kompyuta. Nahitaji msaada wenu na natanguliza shukrani za dhati!!