Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
nimeandika hii thread baada kuangalia mechi ya jana usiku katiya Barcelona na Hercules... kuna mchezaji anaitwa javier Mascherano huyu ni nahodha wa timu ya taifa ya Argentina aliyehamia barcelona akitokea liverpool msimu uliopita kwa madai ya shinikizo la mkewe wake ambaye ni mhispania aliyekua akisema kwamba maisha ya Uingereza hayafurahii kutokana na hali ya hewa ya baridi kali, ndio ikawa sababu kuu ya Mascherano kuhama club ya Liverpool ambapo alikuwa ana namba ya uhakika kikosi cha kwanza na alikuwa anonekana ni kiungo mzuri ambaye kazi yake ilikuwa ni kuharibu mipango ya timu pinzani... na ilifika wakati kocha wa Argentina wakati huo Diego Maradona alisema kwamba yeye mchezaji anayemkubali katika first eleven ni huyu jamaa....... sasa tatizo ambalo lipo sasa ni kwa huyu jamaa kuwekwa benchi kula siku na kocha Pep Guardiola na mbaya zaidi kilichokera mechi ya jana ni kuingiza vichipukizi visivyo na jina akimwacha mascherano nje... je wana JF ambao ni wapenzi wa soka mnalizungumziaje hili la Kapteni wa timu ya taifa kuwekwa bechi katika club yake???....