Nahodha u20 Dickson Job aitwe taifa star

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
Huyu Jamaa ni beki mzuri sana, ameiongoza serengeti boys Garbon, ameiongoza U20 ya mtibwa kuchukua ubingwa kwenye club level.. na sasa ameiongoza national team u20 kuchukua ubingwa wa cecafa.


Wakati kina erasto nyoni na kelvin yondani ndio wanaishia japo wamefanya kaI nzuri.. Beki kama huyu alitakiwa aanze kuitwa kwenye national team.


Naamini kocha na benchi la ufundi watalifanyia kazi la sivyo tutaendelea kuwapigia magoti kina yondani walio maliza muda wao kwa kazi nzuri iliuo tukuka.
 
Wazo zuri, hawa vijana wanatakiwa kujaribiwa na kuwapa uzoefu kwenye mechi za kirafiki. Tatizo letu hata mechi za kirafiki tunataka kushinda tu, hatuangalii maandalizi ya timu kwa manufaa ya mashindano yajayo.

Mechi za kirafiki kocha anaanza na kikosi kilekile cha mashindano, sasa hapo utawapimaje hao walio benchi kila siku kama huwapi nafasi, ndio maana hata kwenye substitutions tunakuwa na wakati mgumu maana tunaowategemea ndio hao wameanza, hakuna option B.
 
Mimi naangalia hilo kombe utafiri la UMISETA kama si UMITASHUMTA, very cheap!!
 
Samahani wandugu nilazima mchezaji asokote nywele vibaya?
 
Sijui kwanini makocha wa timu ya taifa wanamwita kelvin John peke yake
 
Hana refaree ndiyo maana haitwi,Tz kila kitu ni unamfahamu nani
 
Maombi yamejibiwa.. Hongera sana kocha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…