13 September 2022
Nairobi, Kenya
HOTUBA MARA BAADA YA KUAPISHWA NAIBU RAIS MH. RIGATHI GACHAGUA
Naibu wa Rais wa Kenya Mh. Geoffrey Rigathi Gachagua amewaelezea raia wa nchi hii ya Kenya kuwa hali si hali pamoja ya kuwa ni nchi inayohesabika ina uchumi mkubwa na utajiri katika eneo hili la Afrika ya Mashariki lakini awamu hii mpya chini ya rais William Ruto imepokea serikali ambayo imefilisika na naibu rais Geoffrey Rigathi Gachagua bila kupepesa macho amewaambia wananchi waelewe kuwa huo ndiyo ukweli.
Pia pamoja na pigo hilo kukuta fuko la fedha la nchi likiwa tupu huku nchi inadaiwa madeni makubwa lakini chini ya uongozi wa rais wa tano William Ruto watafanya kazi usiku na mchana kuirudisha nchi katika uchumi mzuri na hifadhi ya kutosha ya akiba ya fedha kama ilivyokuwa wakati wa rais Mwai Emilio Kibaki miaka kumi iliyopita yaani 2012.
Anaongeza makamu wa rais Geoffrey Rigathi Gachagua kuwaambia ukweli kuwa wananchi kuwa pia kwa hali ya raia mmoja mmoja kwamba anaelewa hali yao ya kiuchumi ni mbaya, watu milioni 6 hawana ajira huku raia milioni 14 ni wakopaji sugu wenye madeni ya kutisha wanayoshindwa kuyalipa kiasi wameingizwa ktk rejista kuwa hawafai tena kuaminika, lakini kuanzia siku ya kwanza ofisini Rais William Ruto na wasaidizi wake watafanya kila juhudi kurekebisha hali hiyo ngumu na mbaya iliyopo serikalini na kwa wananchi wa kawaida.
Hotuba hiyo ya Naibu wa rais katika awamu hii mpya inayoingia ya rais William Ruto mbele ya maelfu ya watu katika uwanja wa kisasa wa Kasarani jijini Nairobi huku rais anayemaliza muda wake Mh. Uhuru Kenyatta akiwa mita chache akisikiliza kwa makini hotuba hiyo inayochambua awamu iliyopita ya Uhuru Kenyatta.