Naibu Spika afafanua kuhusu Benki na Kampuni za Simu hukata pesa nyingi kuliko Serikali

Mkibadilisha mgawanyo kuna mawili:
1. Bei itabaki pale pale ila ukubwa wa bando utapungua zaidi kufidia gharama, ukumbuke Nape aliwahi kusema wao hawana nguvu ya kudhibiti bei za bando na huo ndio mlango wao wa kutokea.

2. Mitandao isiporidhika wanaweza kuanza kusitisha baadhi ya huduma kama Uber,Bolt walichofanya kwa kisingizio cha gharama za uendeshaji kuwa juu ili kuitia presha serikali warudi katika meza ya mazungumzo.

Vyovyote vile atakayeumia ni mteja wa mwisho, ngoja tuone mchezo utakavyokwenda !
 
Kwa hiyo anataka haya makampuni na mabenki yafanyie biashara serikali!?
 
Toeni tozo mambo yaende,serikali inahitaji pesa
 
Elimu ya ovyo ndio chanzo Cha yote haya watu wanatamka maneno bila hata kufikiria leo huyu kasema hivi kesho yule kasema vile ili mradi ni vurugu mechi ombwe la uongozi kwa Sasa ni kubwa mno
 
Elimu ya ovyo ndio chanzo Cha yote haya watu wanatamka maneno bila hata kufikiria leo huyu kasema hivi kesho yule kasema vile ili mradi ni vurugu mechi ombwe la uongozi kwa Sasa ni kubwa mno
Kwa kweli !!
 
Tatizo la Naibu Spika huwa anaongea vitu ambayo hana tafiti au uelewa navyo.
Nimemsikia mara nyingi ktk upotoshaji mkubwa.
 
Ubinafsi wa wenzetu hawa hawawezi kamwe kuongelea haya Mkuu. Ni mambo ya ajabu kabisa!
 
Hiyo si ni biashara yao, kwani hawawalipi kodi......mnataka kunyonya kwa mrija kwenye biashara za makampuni, kwa kweli viongozi kama hawa wamefilisika akili kabisa.
 
Ndio yalele ya label ya WCB msanii anataka apewe share sawa sawa na Mmiliki wa label diamond
 
Hizi akili kweli kila mtu ana zake !!!!

Kwahio wanataka wakate kiasi gani ? (hawana overheads, research and development n.k.) By the way last time I checked hii ni biashara huria..., watumie bank zao zisicharge iwe bure kabisa ushindani na wenyewe watashusha tu !!!!!

Kwanini wasianze na TTCL na Airtel ambazo wanahisa na kutuonyesha hio business model ?, tena hata wakitaka wachukue 100% Tozo....

Bure Kabisa hawa watu wamesahau kwamba wanaowatumikia ndio hao mwisho wa siku wanaumia kwa hizo Tozo (Wazee wa Kuvuna wasipopanda)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…