Naibu Sipika wa Bunge, Mussa Zungu amewataka wabunge wasiogope kurudi majimboni kwani kuna miradi mingi ya kuzungumzia na kuwa wameonyesha wana sifa za kurudi bungeni 2025.
“Niwapongeze wabunge kwa kazi nzuri mliyofanya kipindi hiki chote ambacho tuko bungeni, mmeonyesha umahiri wenu na mmeonyesha mna sifa za kurudi tena ubunge 2025.
Msiogope kwenda majimboni, nendeni majimboni hiki ni kipindi cha kwenda kuzungumzia faida ambayo tumeipata kutokana na uongozi mahiri wa Rais Samia Suluhu Hassan.
“Mpange maneno ya kwenda kusema jimboni, msiogope. Msiogope wajumbe, msiogope wagombea, mnayo maneno ya kusema msirudi na unyonge, na neno la mwisho ukiishi mbinguni usiogope radi,” amesema Zungu.