Naibu Spika: Watu wanaugua kwa Makelele ya Muziki

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
NAIBU Spika Mussa Azan Zungu ameitaka serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kudhibiti kelele hasa za muziki katika makazi ya watu ambazo zimegeuka kero kwa wakazi.

“Wazee wengi wanateseka na makelele ambayo hayana udhibiti (control). Tuwaombe NEMC mchukue hatua mtoe adhabu kali kwa watu wanaopiga makelele hasa ya muziki,” amesema wakati akiahirisha kikao cha Bunge leo Aprili 24, 2023.

Your browser is not able to display this video.
 
.... "hasa ya muziki"! Kelele ni kelele tu no matter source ni nini! Vyanzo vyote vinavyopitiliza viwango vinavyotakiwa vifungiwe aache unafiki.
 
SIO MUZIKI TU HATA MAKANISA KATI KATI YA MAKAZI NI KERO KUBWA
 
Muziki, Bar, Makanisa, Misikiti.
na mitaani, madukani na sokoni ni kelele tu hasa zile za kuitia biashara, mtu akifungua anawasha kipaza sauti mpaka anafunga. Makanisani na misikitini ni afadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…