Naibu Spika, Zungu: Kuna nyumba za ICU zina chaji Tsh. 500,000 bila dawa

Naibu Spika, Zungu: Kuna nyumba za ICU zina chaji Tsh. 500,000 bila dawa

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu ametoa rai kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)–Hospitali ya Dar Group kutotoza gharama zisizo himilivu kwa wananchi wanaohitaji usaidizi wa huduma za oksijeni.

IMG_5401.jpeg

Kauli hiyo ametoa Julai 29, 2024 wakati wa uzinduzi mtambo wa kisasa wa kuzalisha hewa ya oksijeni wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 500 kwenye Hospitali ya Dar Group, ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Amesema kuna maeneo huduma hizo zimekuwa zikitolewa kwa bei ya juu kwa wenye uhitaji, hivyo ameshauri huduma hizo kuwa himilivu ili kuusaidia Mfuko wa Bima wa Taifa (NHIF) kutokulipa gharama nyingi kwa wagonjwa.

“Kuna nyumba za ICU zina chaji T.Sh 500,000 bila dawa, Mungu ametupa oksijeni na mradi huu uwe sehemu ya kuwapunguzia gharama na wao wapate huduma safi."amesema Zungu

Ameongeza "Tumuige Rais (Samia Suluhu Hassan) shughuli zake ni fupi lakini zina matokea makubwa katika nchi yetu. Tumepata Rais anayependa watu na taifa lake, anahakikisha watu wasipate mahangaiko ya afya."

Akizungumzia huduma hiyo ambayo imezinduliwa, Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk Delila Kimambo amesema mtambo huo unatumia umeme na kuzalisha hewa ya oksijeni yenye ujazo wa milimita za mraba 21 yenye kasi ya mita tano kwa saa wakati wa kujaza.

“Una vifaa vingi ndani yake vikiwemo kifaa cha kupima ubora wa oksijeni, kifaa cha kujaza hewa, tanki la kupokea hewa ina lita 1000 na talinalopokea hewa ya oksijeni wakati wa kutoa lina lita 1000,” amesema.

IMG_5506.jpeg

Aidha Mkurugenzi wa Idara ya afya ya Uzazi, Mama na Mtoto akiwa anawakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya afya, Dk Ahmed Mkawani amesema mtambo huo utaenda kusogeza kwa ukaribu kwa wananchi.

“Wizara inawapongeza kwa kubadili mwonekano wa huduma hapa mmekunza ajira za Watanzania hapa Dar Group na JKCI imeondoa rufaa za nje ya nchi mambo yote ya moyo yanafanyika hapahapa."amesema

Amengoza kuwa uwekezaji unaoendelea kwenye sekta ya afya kwa sasa umefanikisha hospitali zote za rufaa nchini kuzalisha oksijeni jambo ambalo limepunguza changamoto zilizokuwepo awali.
 
Back
Top Bottom