Naibu wa Rais Gachagua ashikwa na kiwewe wakati wa kuapishwa

Naibu wa Rais Gachagua ashikwa na kiwewe wakati wa kuapishwa

Joined
Apr 25, 2013
Posts
19
Reaction score
29
Video ni Naibu wa Rais wa Kenya Mh. Rigath Gachagua mapema siku ya leo amelazimika kurudia tena kuapa baada ya kushikwa na kiwewe hivyo kukosea kuapa. Unadhani ni Kwa Nini Naibu wa Rais wa Kenya Mh. Rigathi alishikwa na kiwewe?.

Disemba 9, 2020 mbele ya Rais Magufuli Naibu Waziri mteule wa Fedha Francis Kumba Ndulane alishikwa na kigugumizi na kushindwa kuapa. Alitenguliwa siku hiyo hiyo na nafasi akapewa mtu mwingine.

Siyo Wizara ya Fedha, alikuwa aape kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Baadaye nafasi yake ilichukuliwa na Profesa Manya ambaye aliteuliwa kuwa Mbunge wa Viti maalumu na baadaye kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Huyu Mbunge aliyeshindwa kuapa alipora Jimbo la Bungara (Bwege).

Ila pia Naibu Waziri wa fedha naye alikuwa akifika mwisho mwa kiapo alikuwa anataja Baraza la Mapinduzi la Zanzibar.
 
Ulimwengu mzima unakuangalia unadhani mchezo!

Ruto ni konki ndio maana hakuwa na wenge!
 
CJ ndiye aliyekosea maana alitakiwa ampatie nakala ya kiapo afuatilie kama ilivyokuwa kwa Ruto. Baada ya CJ kugundua alikuwa hajampa nakala ya kiapo ilibidi ampatie hiyo nakala kwanza ili waendelee na zoezi. CJ aliona busara ni kuanza upya.
 
Alikuwa

CR Sio Cj
 
Yule Mama aliyesimamia kiapo siyo Chief Justice(CJ) yule ni Chief Registrar (CR) kwa kizaramo tunamuita Msajili Mkuu wa Mahakama.

CJ Koome alisoma waraka wa kumthibitisha Ruto kuwa ndiye mshindi wa kiti Cha Rais wa Jamhuri ya Kenya.
CJ ndiye aliyekosea maana alitakiwa ampatie nakala ya kiapo afuatilie kama ilivyokuwa kwa Ruto. Baada ya CJ kugundua alikuwa hajampa nakala ya kiapo ilibidi ampatie hiyo nakala kwanza ili waendelee na zoezi. CJ aliona busara ni kuanza upya.
 
Ingekuwa nchi fulani miaka ile, ungesikia nabadilisha namweka mtu mwingine.
 
Back
Top Bottom