Kenyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 414
- 314
Naibu wa Rais Rigathi Gachagua leo amefunguka na kukiri kuwa serikali inapitia wakati mgumu katika kuwalipa wafanyakazi wake na hata kutoa fedha kwenda kwa serikali za kaunti, kutokana na uhaba wa fedha.
"Ni kweli kabisa kuwa tunatatizika kulipa mishahara na hata kutoa pesa kwenda kwa kaunti, kwa sababu serikali iliyopita ya 'handshake' ilipora kila kitu. Hamna chochote.'
Gachagua amefichua haya huku Wabunge na Maseneta wakizidi kulalama kuwa wangali bado kupokea mishahara yao ya mwezi Machi.
Aidha huduma nyingi zimesimama katika kaunti nyingi kwani serikali kuu bado haijatoa fedha kwenda kwa kaunti.
Duru zinasema walioko mishahara ya mwezi Machi ni Walimu , maafisa wa Jeshi la Polisi pamoja na maafisa wa Jeshi la Ulinzi KDF.