Naibu wa Rais Rigathi Gachagua awahi ofisini saa 11 alfajiri kwa siku ya 3 mfululizo

Kenyan

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
414
Reaction score
314
Naibu wa Rais Rigathi Gachagua leo kwa mara nyingine tena alifika ofisini kwake, Harambee House, saa kumi na moja alfajiri na kama ilivyo ada alichapisha picha kwenye ukurasa wake wa Twitter akitoa Rai kwa wananchi kupambana katika kazi zao za Kila siku. Aliandika:

"Kenya ni taifa la wapambanaji. Tusikubali yeyote atuondoe humo. Tuchapeni kazi."

Ikumbukwe Gachagua ndiye Bosi wa nchi muda huu baada ya Rais William Ruto kuondoka nchini yapata siku tatu zilizopita kwa ajili ya ziara ya kikazi nchini Ujerumani na Ubelgiji.

Aidha kumbuka pia Leo Alhamisi ni siku nyingine ambapo maandamano yanayoongozwa na Raila Odinga yanatarajiwa kufanyika, huku Polisi wakipigia doria katika maeneo tofauti ya nchi hasa Jiji la Nairobi na kaunti zilizoko Kanda ya Ziwa.

Your browser is not able to display this video.
 
Anawahi kazini ku tweeet na kutizama wakenya wakoongea nini kwa twiti yake
 
 
Yeye anawahi asubuhi Sana zile siku za maandamano..Hana la maana zaidi ya kupanga kutukana uhuru kila siku na kutuma watu wakaharibu Mali za uhuru...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Huyu ni nduli, ni ile type ya viongozi wa miaka 50 iliyopita ,hafai kuongoza Kenya
 
Mwizi wa pesa za county ya Kwale, kuna siku hatafiki tena ofisini, nakuhakikishia siku zake zinahesabika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…