Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Kuelekea miaka 50 ya Shule ya Sekondari Jitegemee, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Denis Londo amewataka wananchi wakiwemo viongozi mbalimbali waliowahi kusoma katika shule hiyo ya jeshi kuunganisha nguvu kuwezesha maboresho ya miundombinu ya shule hiyo inayoonekana kuwa chakavu.
Naibu Waziri, Mhe. Denis Londo ametoa rai hiyo mkoani Dar es Salaam ambapo amesema Jitegemee imekuwa na mchango mkubwa katika Taifa, sio tu katika kutoa elimu ya nadharia bali kuwajenga vijana kuwa wakakamavu wakiwemo viongozi wenye uzalendo na nchi yao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule hiyo, Kanali Robert Kessy amesema shule itandelea kuwa mfano bora katika kutoa elimu inayolenga kumkomboa mtoto wa Kitanzania, sio tu kitaaluma bali hata kimaadili.
"Baadhi ya viongozi waliopo katika utumishi serikalini na sehemu mbalimbali ya nchi wametokana na maelezi yanayotolewa kwenye shule za jeshi ikiwemo hii ya Jitegemee," amesema Kanali Kessy.
Kilele cha Maadhimisho hayo ya Miaka 50 ya Jitegemee Sekondari kinatarajiwa kuwa Novemba Mosi, 2024 katika sherehe ambazo zitaambatana na harambee ya kuchangia maboresho ya miundombinu ya shule hiyo.