Naibu Waziri Godwin Mollel amuunga mkono Chalamila kuhusu wajawazito: Unakuta mtu hana bima lakini anachangia Milioni kwenye harusi!

Naibu Waziri Godwin Mollel amuunga mkono Chalamila kuhusu wajawazito: Unakuta mtu hana bima lakini anachangia Milioni kwenye harusi!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akijibu swali la Mbunge wa viti Maalumu, Anatropia Lwehikila Theonest amezungumzia kauli ya RC Chalamila akisema:

"Suala alilozungumzia ni nyeti mno, suala la akina mama na mambo mengine ya dharula tunatoa maelekezo mahususi kwanza moja kwa hospital za private lakini pia za umma kwamba mama na mtu mwingine yoyote wa dharula kwamba kwanza apate huduma sio suala la kuuliza fedha.

Soma: Mbunge ahoji kauli ya serikali kuhusu wanawake wanaokosa vifaa vya kujifungulia, Naibu waziri asema huduma kwanza na si kuulizwa pesa

IMG_0280.jpeg
"Ni kwamba huduma kwanza mambo mengine baadaye lakini niwaambie waheshimiwa wabunge kwenye hili eneo la akina mama na watoto tunajua sisi wenyewe tumepitisha Bilioni 200 kwa ajili ya dawa lakini ukipiga gharama za mwaka za kutibu akina mama na watoto kwa mwaka ni Bilioni 227 na sisi tumetenga kwa huduma zote ni Bilioni 200 kwahiyo kunakuwa na hatua mbali mbali zinafanywa ili kubalance hizo hela"

"Na tunao watu wengi kule lakini unakuta mtu huyo huyo hana bima hana chochote lakini anachangia Milioni kwenye harusi, lakini ikifika suala la mke wake kujifungua hana hizo fedha anataka aseme asaidiwe bure
 
Mkeka wa mama unasukwa,hawa wpte OUT,rwturn to sender
 
QmmmmmQe zao
Hao wanaochangia milioni kwenye hharusi ni high class ambao huwezi kukuta wamejazana Mwananyamala, hivyo huyo naibu waziri ni mjinga kama wajinga wengine.
Kaongea upuuzi
 
Niliandika hapa Chalamila alitumwa kuyasema yale watu wakanishukia vibaya mno. Isingewezekana Chalamila atoe maelekezo na ufafanuzi wa jambo kubwa na nyeti kama lile bila ruhusa ya bosi wake.
 
Mnawaonea bure Chalamila na Mollel.
Shida ilianzia kwa Trump.
Mnataka wao wafanyeje ilhali Trump amekata misaada?
 
Kuna Muuza mboga au vitumbua anayetoa mchango milioni kweli? Shughuli zetu za laki tati none na kuipata Mtoto labda kama uwe unajuana na Waziri au Mbunge ndio akupe milioni.
 
Niliandika hapa Chalamila alitumwa kuyasema yale watu wakanishukia vibaya mno. Isingewezekana Chalamila atoe maelekezo na ufafanuzi wa jambo kubwa na nyeti kama lile bila ruhusa ya bosi wake.
Je huyo Mama yupo kweli au hii ilikua mpango mkakati wa kuleta msg flani!? Maana mlalamikaji haonekani lakini Chalamila ndiyo kama yeye ndiyo mtendewa!!
 
📌📌📌KAMA HUNA HELA FUNGA KIZAZI

TRUMPET AMEKAZA VYUMA HUKO,HAKUNA BURE WALA MJOMBA WAKE NA BURE!!!
 
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akijibu swali la Mbunge wa viti Maalumu, Anatropia Lwehikila Theonest amezungumzia kauli ya RC Chalamila akisema:

"Suala alilozungumzia ni nyeti mno, suala la akina mama na mambo mengine ya dharula tunatoa maelekezo mahususi kwanza moja kwa hospital za private lakini pia za umma kwamba mama na mtu mwingine yoyote wa dharula kwamba kwanza apate huduma sio suala la kuuliza fedha.

Soma: Mbunge ahoji kauli ya serikali kuhusu wanawake wanaokosa vifaa vya kujifungulia, Naibu waziri asema huduma kwanza na si kuulizwa pesa

View attachment 3219806"Ni kwamba huduma kwanza mambo mengine baadaye lakini niwaambie waheshimiwa wabunge kwenye hili eneo la akina mama na watoto tunajua sisi wenyewe tumepitisha Bilioni 200 kwa ajili ya dawa lakini ukipiga gharama za mwaka za kutibu akina mama na watoto kwa mwaka ni Bilioni 227 na sisi tumetenga kwa huduma zote ni Bilioni 200 kwahiyo kunakuwa na hatua mbali mbali zinafanywa ili kubalance hizo hela"

"Na tunao watu wengi kule lakini unakuta mtu huyo huyo hana bima hana chochote lakini anachangia Milioni kwenye harusi, lakini ikifika suala la mke wake kujifungua hana hizo fedha anataka aseme asaidiwe bure
Nchi iuzwe tu..kila mtu apewe Chake .sio kwa dharau hizi kwa raia
 
Back
Top Bottom