Naibu Waziri Godwin Mollel: ARV zinaendelea kupatikana bure kwa wagonjwa wote nchini

Naibu Waziri Godwin Mollel: ARV zinaendelea kupatikana bure kwa wagonjwa wote nchini

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
655A1311.JPG
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, amesema kwamba serikali imeendelea kuhakikisha huduma za upatikanaji wa dawa (ARV) za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI zinaendelea kupatikana bila malipo kwa wagonjwa wote.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 20, 2025 alipoungana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy deriananga, na viongozi wengine na wadau katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya Mradi wa Timiza Malengo uliofanyika mkoani Lindi.

Dkt Mollel amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeboresha sekta ya afya kwa kiasi kikubwa ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya afya ambapo serikali imetumia kiasi cha zaidi ya bilioni 48 kwenye ujenzi wa miundombinu peke yake kama vile hospitali, vituo vya afya na zahanati katika mkoa wa Lindi.

Dkt Mollel akizungumzia upatikanaji wa huduma za afya za kibingwa amesema, "Hapo mwanzo zilikuwa hazipatikani katika nchi yetu lakini kwa sasa zipo Tanzania, mfano matibu ya uvumbe wa ubongo bila kupasua kichwa sambamba na matibabu ya kansa ya ubongo kwa kutumia sauti maalumu,".

Mradi wa TIMIZA MALENGO awamu ya tatu unatekelezwa katika halmashauri 36 katika mikoa 10 ya Tanzania Bara ambayo ni Dodoma, Geita, Lindi, Mara, Morogoro,Njombe, Ruvuma, Singida,Tabora na Tanga.

===============​

Waziri Molel Ashiriki Uzinduzi wa Mradi wa Timiza Malengo, Ataja Mambo Makuu ya Dkt.Samia Sekta ya Afya.

Naibu Waziri wa afya Dkt.Edwin Molel leo tarehe 20.02.2025 ameungana na Mhe. Ummy Hamis Nderiananga, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) na viongozi wengine na wadau katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya Mradi wa Timiza Malengo.

Akizindua mradi huo Mhe.Ummy Ndeliananga amesema katika amesema UKIMWI unachangia katika kushuka kwa Uchumi wa nchi na kuongezeka kwa umasikini hivyo, serikali imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo Upimaji wa VVU, matumizi ya Kondomu na afua za Matibabu kwa watu wanaoishi na VVU.

Nae Mhe. Edwin Molel (Mb) amesema serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imeboresha sekta ya afya kwa kiasi kikubwa na amebainisha maeneo manne makubwa:-
655A1320.JPG
Ujenzi wa miundombinu ya afya ambapo Serikali ya Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetumia kiasi cha zaidi ya bilioni 48 kwenye ujenzi wa miundombinu peke yake kama vile hospitali, vituo vya afya na zahanati katika Mkoa wa Lindi

Pili Dr. Molel amezungumzia upatikanaji wa huduma za afya za kibingwa ambazo apo mwanzo zilikuwa hazipatikani katika nchi yetu lakini kwa sasa zipo Tanzania. Mfano matibu ya uvumbe wa ubongo bila kupasua kichwa sambamba na matibabu ya kansa ya ubongo kwa kutumia sauti maalumu.

Pia alieleza namna Tanzania inavyotambulika kimataifa kwa hatua kubwa iliyofikiwa katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kinamama na pia vifo vya Watoto wachanga. Mabadiliko haya ni ndani ya kipindi kifupi cha miaka minne tu.

Mwisho aligusia upatikanaji wa matibu bure kwa wagonjwa wanaoishi na maambukizi ya VVU. Mheshimiwa naibu Waziri amesema Mheshimiwa Rais Pamoja na Serikali yake amehakikisha huduma za kupunguza makali ya VVU zinapatikana bila malipo kwa wagonjwa wote .

Mradi wa TIMIZA MALENGO awamu ya tatu unatekelezwa katika halmashauri thelathini na sita 36 katika mikoa kumi ya Tanzania Bara ambayo ni Dodoma, Geita, Lindi, Mara, Morogoro,Njombe, Ruvuma, Singida,Tabora na Tanga.
 
Back
Top Bottom