Naibu Waziri Kapinga: Bado Vijiji 151 tu Nchi nzima kufikiwa na umeme

Naibu Waziri Kapinga: Bado Vijiji 151 tu Nchi nzima kufikiwa na umeme

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Nawakumbusha tu kwamba Bado Vijiji 151 Tanzania nzima kuwa na umeme na kati ya hivyo Wakandarasi wako site.
---

1721485008850.png
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema vijiji 151 tu nchi nzima ndio ambavyo bado havijafikiwa na huduma ya umeme kati ya vijiji zaidi ya 12,000 ambapo wilayani Ludewa mkoani Njombe vimebaki vijiji nane.

Kapinga ameyasema hayo jana tarehe 19 Julai 2024 wakati wa ziara ya kikazi katika Vijiji vya Lubonde na Maweni wilayani Ludewa mkoani Njombe akikagua miradi ya nishati.

Wakati wa ziara hiyo Kapinga alifanikisha kuingiwa makubaliano kati ya Kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya Madope iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ya kukabidhi miundombinu ya kusafirisha na kusambaza umeme kwa Shirika hilo baada ya kusainiwa kwa mkataba kati ya pande hizo mbili.

Kapinga amesema kuwa Serikali inathamini kazi kubwa inayofanywa na Kanisa Katoliki kwa kushirikiana na Serikali kwenye uwekezaji katika sekta mbalimbali.

My Take
Hata hili Machadema yatapinga na kusema hakuna kilichofanyika chini ya CCM.

Mkosoe Rais Samia Kwa mambo mengine sio delivery ya Maendeleo.

View: https://twitter.com/AnnaSarungi/status/1815308723377627145?t=m85dXmJsgq3IRy4YX9QdXA&s=19
 
Waziri unakwama wapi wajua Tanzania ina ukubwa wa square mita laki 9 ama hata msongo wa umeme mkubwa ukipita tayari wanasema umeme upo
Nani anaesema hayo? Swala ni vijiji vilivyofikiww na umeme.

Kwa taarifa Yako hata maji ya Bomba kufikia mwakani 2025 karibia kila.kijiji Kitakuwa na maji ya Bomba ,Hadi mwezi machi ilikuwa Bado Vijiji chini ya 2,000
 
Here vitajeni hivyo vijiji kwa majina ili tuangalie tuone ni kweli ni hivyo 151 au kuna zqidi.

Wanasiasa siwaamini,
Lakini shida moja umeme unaweza kufika shuleni tu na nyumba labda 3 tu,issue wananchi wengine kuupata ni lazima wanunue nguzo kwahiyo wanashindwa kuupata badala yake unabaki shuleni tu au hospitali.
Tanesco waje na mpango wa kukopesha kuunganishia wanakijiji na watakuwa wanawakata Kadri wanavyonunua umeme.
Kama makampuni yanaweza kukopesha wananchi kuanzia 2,000,000 Sola pamoja na TV kwa wananchi serikali inashindwa nini kumkopesha mteja ambaye atatumia umeme maisha yake yote?
Kama umeme Tanzania tunao wakutosha tunakosa plan ya kuusambaza ili wananchi wote waupate siyo kusema vijiji tu.vijiji hilivyofikiwa ni taasisi za serikali tu siyo wananchi wenyewe..
Wafikishieni wananchi umeme na kuwakopesha majiko ya kupikia ili kuokoa mistu wasitumie kuni na mkaa .
 
Kwa Sasa wamepewa ofa ya km 2 za Bure Kila Kijiji hapo hawatachangia chochote zaidi ya wiring ya nyumbani kwao na Ile 27,000
 
Mbona hawatangazi? Mameneja wa wilaya wanajua? Mbona hawatangazi? Wananchi wakienda kuomba wanaambiwa mwisho mita 30 kutaokq kwenye nguzo uanlipia 27,000 ikizidi hapo unatozwa nguzo zinazozidi Kwa namna hii umeme watu watausikia tu vijijini. Watangazie wananchi kama watashindwa kuunganisha.leo ndiyo nimesikia kwako hiyo offer ya kilometa 2
 
Ndio utaratibu
 
Umeme hautumiwi na wanavijiji kutokana na umaskini uliotopea. Vijiji vingi umeme unawaka kwenye ofisi ya kijji tu
 
Ukienda kuomba unaambiwa mitaa mingine wasubiri mradi mwingi phase 1 imeisha kama unataka zaidi ya mita 30 ujigharimie nguo wewe mwenyewe
 
Back
Top Bottom