Naibu waziri Katambi apiga marufuku tabia za watumishi wa umma kubagua watu wenye ulemavu

Naibu waziri Katambi apiga marufuku tabia za watumishi wa umma kubagua watu wenye ulemavu

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi amekemea tabia za watumishi wa umma kubagua watu wenye mahitaji maalum wakati wanapohitaji huduma kwenye ofsi zao.

Amekemea tabia hizo wakati wa maadhimisho ya siku ya maandishi ya nukta nundu kitaifa yakifanyika mkoani Tabora ambapo amesema mtumishi yeyote mwenye tabia za kibaguzi hatavumiliwa.

Katika risala iliyosomwa na Bw Donatus Rupoli akiwakilisha umoja wa watu wasiyoona nchini TAB imebainisha kuwa miongoni mwa changamoto wanazokumbana nazo nipamoja na kutozingatiwa katika mikakati ya serikali kama ilivyo kwa wenye ulemavu mwingine.

 
Back
Top Bottom