Naibu Waziri Katimba Atoa Maelekezo kwa Chuo cha Hombolo Kuwajengea Uwezo Viongozi wa Mitaa na Vijiji

Naibu Waziri Katimba Atoa Maelekezo kwa Chuo cha Hombolo Kuwajengea Uwezo Viongozi wa Mitaa na Vijiji

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba ametoa maelekezo kwa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo kuwasiliana na Wakurugenzi Halmashauri zote nchini ambazo hazijatimiza maelekezo ya serikali ya kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa serikali za mitaa na vijiji ili wawezeshe kupata mafunzo hayo.

GkIu3ESW8AAYgsp.jpg
Mhe. Katimba ametoa maelekezo hayo baada ya kutembelea chuo hicho kilichopo Hombolo jijini Dodoma ikiwa ni ziara ya kikazi ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na viongozi na watumishi wa taasisi hizo ili kupata mwelekeo wa kiutendaji wa Taasisi hizo.

"Mafunzo haya ni ya lazima sio ya hiari mfanye mawasiliano ili waweze kuhakikisha mafunzo haya yanaweza kufanyika kwa wenyeviti wetu hawa na mafunzo haya mnayotoa yana lengo zuri la kuwajengea uwezo wale watendaji wote waliopo huko kwenye mamlaka za serikali za mitaa waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi," amesema

GkIu3ETXcAE3Hiw.jpg
Amesisitiza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi yanatakiwa kuendana na mabadiliko ya kifikra ili mamlaka za serikali za mitaa zielewe kuwa pamoja na utoaji wa huduma kwa jamii bali ni chombo cha kuwezesha shughuli za kiuchumi.

"Mamlaka zetu za serikali za mitaa ziwe ni chombo cha kuchochea na kuwezesha wananchi katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali katika sekta mbalimbali najua mna'component' nyingi lakini katika eneo hili natoa msisitizo,"amesema Mhe. Katimba

GkIu3ETWkAA31FU.jpg
GkIu3EMWsAATkH1.jpg
 
Kheeeh huyu dada hiki cheo kapewa lini? Dooh
 
Back
Top Bottom