Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
CHILO: HUDUMA YA MAJI 🚰 💦 SAFI NA SALAMA ITAFIKA KILA PAHALA KATIKA JIMBO LA UZINI
Mbunge wa Jimbo la Uzini KHAMIS HAMZA CHILO amewahakikishia Wananchi wa Jimbo la Uzini kua HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA ITAFIKA KILA KONA YA JIMBO LA UZINI
Muheshmiwa KHAMIS CHILO ameyasema hayo alipokua akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Koani COSOVO katika Shehia ya Koani Wadi ya Koani Jimbo la Uzini Mara baada ya Kufungua na Kuzindua Mifereji ya Maji safi na Salama kwa Wananchi wa Kijiji hicho
Muheshmiwa KHAMIS CHILO amesema asili ya Mifereji hiyo ni Ziara zake za Kupita na Kusikiliza kero na Changamoto za Wananchi katika kijiji hicho ambazo alizifanya Mwaka jana
Aliwaambia kua Mama Samia na Dr Mwinyi ndani ya Jimbo la Uzini wametupatia Bilion 2.3 kwa ajili ya Ujenzi wa Miladi Mikubwa ya Maji safi na Salama na Wametujengea Matangi makubwa mawili ya kisasa ya Maji ambayo moja lipo Bambi na Jengine lipo Mgeni Haji kila moja lina Ujazo wa Lita Milion Moja matangi hayo Yatasambaza Maji katika Shehia zote za Jimbo la Uzini hiyo ni kazi kubw ilioyofanywa na Viongozi wetu tuna kila sababu ya Kuwapongeza na Kuwashukuru pia ...👏🏽👏🏽
Aidha Muheshmiwa KHAMIS CHILO amewataka Wananchi hao Kuitunza na Kuihifadhi Miundambinu hiyo ili iweze kuwafaa na Kudumu kwa Muda Mrefu kwani Imetumia garama kubwa mpaka kukamilika kwake..
Muheshmiwa KHAMIS CHILO amewataka Wananchi hao Kuendelea kua na Imani na Viongozi wao wakiwemo Mbunge, Mwakilishi na Madiwani kwani wanafanya kazi Kubwa ya Kuwatumikia Wananchi kwenye Jimbo la Uzini....
Muheshmiwa KHAMIS CHILO Amesema kwa sasa Viongozi ni wao kwa hiyo bado wana wajibu wa Kuendelea kuwatumikia Wananchi wao bila ya Kujali Itikadi, Asili, Jinsia au Kabila maana waliwachagua kwa imani
Muheshmiwa KHAMIS CHILO amesema katika Kijiji cha Koani wamefanya Mambo mengi sana na Makubwa ya Kuweka Alama kama Vile Daraja Kibonde Maji Ambalo Limegarimu Milion 26, Shule ya Koani ambayo Imegarimu Milion 16, Kisima Koani Manyame Kimegarimu Milion 8, Ukarabati wa Soko la koani Limegarimu Milion Moja, Ligi za Vijana, Tanki za Msikiti Wa Mwera Minazi Mikinda, Ujenzi wa Skuli ya Mwera ya Ghorofa(UVICO),Mashine ya Maji kwenye Bonde la Mpunga Koani Imegarimu laki tano..
Muheshmiwa KHAMIS CHILO amesema Koani kwa kiasi chao Wamefanya mambo mengi na makubwa sana hivo anawataka Wananchi waendelee kua na Imani na yeye kwakua bado hajawatupa na yupo karibu nao...
Nae Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Muheshmiwa HAJI SHABAN WAZIRI amesema Utekelzaji wa Ilani haswa kwenye Sekta ya Maji safi na Salama Tuliahidi wakati tunapita tunaomba Kura kwa Wananchi na Loe Tumetekeleza kwa Vitendo
Na aliwaahidi wengine wa Maeneo Mengine kua Wawe na Subra Huduma ya Maji Itafika ...
UZINI HATUPOI KAZI INAENDELEA