Naibu Waziri Kihenzile amuongoza Rais wa Guinea Bissau, Umaro Embalo Kktembelea Mradi wa Treni ya Kisasa ya SGR

Naibu Waziri Kihenzile amuongoza Rais wa Guinea Bissau, Umaro Embalo Kktembelea Mradi wa Treni ya Kisasa ya SGR

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Mwakiposa Kihenzile alimpokea Rais wa Guinea Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embalo akiwa Kiongozi wa kwanza kutembelea Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR ya Dar es Salaam - Morogoro ambayo imeanza rasmi tarehe 14.06.2024 ambapo wamesafiri naye toka Dar mpaka Pugu kwa treni.

Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló atembelea mradi wa reli ya Kisasa ya SGR kwa kutumia treni ya Kisasa ya reli hiyo kutoka stesheni ya Dar es Salaam hadi stesheni ya Pugu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.

Rais Mhe. Embalo amefurahishwa sana na hatua kubwa ambayo Taifa letu limepiga kwenye miundombinu ya Reli ya Kisasa. Reli ya SGR Kipande cha kwanza mpaka cha saba kutoka Dar mpaka Mwanza mpaka Kigoma kisha Msongati-Gitega, Burundi ikikamilika itapelekea Tanzania kuwa na kilometa takribani 2,300 na kuwa nchi ya tano duniani kwa kujenga Reli ndefu zaidi duniani na kuwa Nchi ya kwanza kwa Nchi zinazoendelea.

Nchi zenye reli ndefu Duniani ni pamoja na China km 40,493, Hispania km 3719, Japan 3146, Ufaransa Km 2735. Nchi zingine ni Uturuki Km 1631, Finland 1232 na 1120.

PIA SOMA

- Rais Samia kumpokea Rais wa Guinne Bissau Ikulu hapo kesho

GQvIaFVWUAECWFI.jpg
GQvIaFPX0AAbzJm.jpg
GQvIaFOXwAA6_lM.jpg
GQvIaFUXMAApHQh.jpg
Screenshot 2024-06-24 at 17-24-39 David Mwakiposa Kihenzile (@david_mwakiposa_kihenzile) • Ins...png
Screenshot 2024-06-24 at 17-24-47 David Mwakiposa Kihenzile (@david_mwakiposa_kihenzile) • Ins...png
 
Mbona waziri wa Mambo ya nje yupo. Marekani wana kama ngapi za reli na urusi na canada?
 
Back
Top Bottom