The Sunk Cost Fallacy 2
JF-Expert Member
- Nov 8, 2022
- 9,436
- 10,944
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati bwana Dotto Biteko amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Imefuta zaidi ya tozo na kero 370 Kwa lengo la kukuza biashara na uwekezaji Nchini.
Bwana Biteko amesema hatua hiyo imechochea kukua Kwa biashara na uwekezaji Nchini akitolea mfano ongezeko la mahitaji ya umeme ya zaidi ya megawatt 400 ndani ya mwaka mmja Kwa na kufanya mahitaji kuongeza kutoka megawatt 1400 Hadi 1900 Kwa sababu ya uhitaji mkubwa wa umeme kwenye sekta ya viwanda.
==
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko, alisema hayo jana Dar es Salaam alipokuwa akifungua Kongamano la Majadiliano ya Biashara na Uwekezaji Kati ya Serikali na Sekta Binafsi na Mkutano Mkuu wa 49 wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA).
Alisema kufutwa kwa tozo hizo kumepunguza Sh. bilioni 35 kwenye mapato ya serikali kwa mwaka na kwamba imefanya hivyo baada ya kusikiliza kero za wafanyabiashara.
Pia alisema serikali imepunguza muda wa kutoa huduma kutoka simu 14 hadi tatu na usajili wa hospitali binafsi, kutoka miezi 12 hadi siku tatu.
Alisema lengo la serikali kufanya hivyo ni kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, ili kuchochea ukuaji wa uchumi.
Dk. Biteko alisema serikali imefanya hivyo ili kuongeza mzunguko wa biashara ambao utaongeza mapato ya kodi, itakayotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na huduma za kijamii.
Alisema mbali na maboresho hayo, serikali imeimarisha bandari na miundombinu mingine, ikiwamo ujenzi wa barabara, meli, reli ya kisasa na ununuzi wa ndege ya mizigo.
Maboresho hayo, alisema yameongeza mahitaji ya umeme kutoka megawati 70.8 mwaka 2017/18, hadi megawati 420 mwaka huu.
“Mahitaji ya juu ya umeme Agosti mwaka jana yalikuwa megawati 1,410 lakini leo ni MW 1,888, ongezeko hili limekuja kwa sababu viwanda vingi vinajengwa na uchumi unachangamka,” alisema.
Dk. Biteko alisema serikali inatambua mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi na kuwashauri wanachama wa TCCIA, kutumia malighafi za ndani katika kuzalisha bidhaa zenye ubora, zitakazoweza kushindana sokoni.
“Mchango wa sekta binafsi ni mkubwa na hauwezi kupuuzwa. Vijana zaidi ya milioni 12 wanaingia kwenye soko la ajira kila mwaka, asilimia 25 ndio wanapata ajira katika sekta rasmi. Asilimia 75 wanaingia katika sekta isiyo rasmi mkiwamo ninyi," alisema Dk. Biteko.
Rais wa TCCIA, Vicent Minja, alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua nchi na kutatua changamoto za biashara.
Hata hivyo, aliomba mchakato wa kuandika sera ya sekta binafsi uharakishwe ili kuiweka kwenye mpangilio unaohitajika.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisema dhamira ya serikali ni kuendelea kuifungua nchi na kuendeleza uhusiano mzuri na sekta binafsi ili kukuza uchumi wan chi.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA, Oscar Kissanga, alitia saini mikataba minne ya ushirikiano na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Wakala wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Kongani ya Viwanda Kibaha.
TCCIA ina zaidi ya wanachama 30,000 na katika mkutano wa jana, wawakilishi 350 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara walikuwapo.
Chanzo: Nipashe
My Take: Hongera sana Rais Samia,hakika wewe ni pro Business Leader,na bila shaka mambo yatakuwa Mazuri zaidi pindi Jopo la mapitip ya kero za Kodi na tozo ulilounda likitia ripoti yake.
Hakika yajayo yanafurahisha.