Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu: Njombe, Iringa na Mbeya maambukizi ya VVU bado yapo juu

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu: Njombe, Iringa na Mbeya maambukizi ya VVU bado yapo juu

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Hivi hii mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya kuna shida gani?

Mbona kila siku maambukizi yako huku tu?

Akiwa anazungumza hivi karibuni ambaye ni Naibu Waziri-Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera Bunge na uratibu alisema:

"Bado kuna mikoa ina ushamiri mkubwa wa VVU kwa mfano Njombe, Iringa na Mbeya ina ushamiri mkubwa zaidi lakini mkoa wa Kigoma una ushamiri mdogo zaidi"

Pia amesema kiwango cha Maambukizi ya VVU kwa watu wenye umri kuanzia Miaka 15 - 45 kimepungua kidogo, kutoka asilimia 4.7 Mwaka 2017 hadi asilimia 4.4 Mwaka 2023.





====================================​

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Deriananga amesema bado kuna mikoa yenye ushamiri mkubwa wa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU), ametoa mfano Njombe una Asilimia 12.7, Iringa 11.1%, Mbeya 9.6%, upande wa Kigoma una maambukizi ya kiwango cha chini ambacho ni chini ya 1.7%.

Pia amesema kiwango cha Maambukizi ya VVU kwa Watu wenye umri kuanzia Miaka 15 - 45 kimepungua kidogo, kutoka 4.7% Mwaka 2017 hadi 4.4% Mwaka 2023.

Upande wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, Dkt. Catherine Joachim amesema Watu Milioni 1.7 wanaishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI Nchini na takribani Watu elfu 60 wanapata maambukizi hayo kila mwaka.

Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa TIMIZA MALENGO awamu ya tatu unaotekelezwa katika Halmashauri 36 katika mikoa 10 ya Tanzania Bara ambayo ni Dodoma, Geita, Lindi, Mara, Morogoro,Njombe, Ruvuma, Singida,Tabora na Tanga.
 
Hiyo mikoa ni route kubwa ya usafiri Tanzania.

Madereva wa malori hawabebi mizigo tu, mpaka virus.
 
Mikoa hiyo ina baridi sana. Serikali iondoe kodi na ihamasishe wananchi kufunga heaters kwenye nyumba zao. Umeme uko kila mahali.
 
Uko serious?
I am serious of course. Hali mbaya ya hewa (baridi kali) inaonekana kuwa factor mojawapo ya maambulizi unlike mikoa yenye joto. Ushauri wangu ni kujaribu ku-weaken hiyo factor. Au nimekosea ndugu yangu?
 
Back
Top Bottom