Naibu Waziri Pinda: Hekima itumike kutatua migogoro ya familia inayohusu ardhi

Naibu Waziri Pinda: Hekima itumike kutatua migogoro ya familia inayohusu ardhi

Joined
May 14, 2024
Posts
94
Reaction score
75
HEKIMA ITUMIKE KUTATUA MIGOGORO YA FAMILIA: NAIBU WAZIRI PINDA

Na. Joel Magese, ROMBO

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amewataka Watanzania kutumia hekima katika kupata suluhisho la migongano ya kifamilia inayohusu ardhi kabla ya kufika mbele ya vyombo vya kisheria.

Naibu Waziri amesema hayo Septemba 18 2024 katika Klinik ya Ardhi iliyofanyika Soko la Mbomai Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro ambapo alipata wasaa wa kuwasikiliza wananchi juu ya kero mbalimbali za ardhi.

Akiwa katika eneo hilo, Naibu Waziri Pinda amewahimiza wananchi kuanza kutafuta suluhu za migogoro ya ardhi inayozikabili familia zao huku akisisitiza hekima kutumika katika kupata suluhisho la migogoro kabla ya kufika mbele ya vyombo vya kisheria.

Ameeleza kuwa, kinachopandwa kuhusiana na migogoro ya kifamilia hakitaishia kwao bali itakuwa ni laana ya kizazi kizima na watoto watarithi na wale wasiolijua jambo linalogombaniwa watakuwa hatari zaidi.

"Mnachokipanda hakitaishia kwenu, itakuwa laana ya kizazi kizima na watoto watarithi na wale wengine wasiolijua jambo lenyewe watakuwa hatari zaidi, acheni kugombana, tumieni vikao jamani " alisema mhe. Pinda.

Naibu Waziri Mhe. Pinda yuko katika ziara ya kikazi mkoni Kilimanjaro ambapo mbali na mambo mengine atasikiliza na kutatua changamoto za ardhi kwa wananchi wa mkoa huo.

Soma Pia: Msiuze maeneo ya wazi - Pinda

-‐---------Mwisho-----------
 
Back
Top Bottom