Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Serikali imezindua Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia mkoani Pwani, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha haki inapatikana kwa wananchi wote, hususan wale wenye changamoto za kisheria lakini wasio na uwezo wa kugharamia huduma hizo.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo Februari 24,2025 katika Kata ya Maili Moja, Uwanja wa Stendi ya Zamani, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Jumanne Sagini amesema kuwa serikali imejipanga vyema katika utekelezaji wa kampeni hiyo, ambapo huduma zitaanza kutolewa kuanzia Februari 25 hadi Machi 5, 2025.
"Wizara imejipanga kwa dhati katika utekelezaji wa kampeni hii, na mara baada ya uzinduzi tutaanza kutoa huduma hizo katika mkoa wa Pwani kuanzia kesho, huduma zitakazotolewa ni pamoja na utoaji wa elimu ya kisheria, utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, kuandaa nyaraka za kimahakama, kuwakilisha wananchi kwenye vyombo vya utoaji haki, pamoja na ushauri wa kisheria," amesema Sagini.
Amefafanua kuwa kampeni hiyo itatekelezwa katika kata 10 za mkoa wa Pwani, ambapo kila kata itajumuisha vijiji au mitaa isiyopungua mitatu, hivyo kufikia vijiji 30 kwa kila halmashauri.
Source: Nipashe