Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Naibu Waziri Waji, Kundo amechukizwa na kucheleshwa kwa mradi wa maji,
Mradi uko asilimi 12.8 na mkadarasi hana uhakika kama Certificate wamesharise, Mkandarasi kasema mpaka acheki na ofisi, Waziri wa maji amemuhoji kuwa kasema yeye ni Eng. ila hata kuraise Certificate hajui mpaka acheki na ofisi.
Mkandari amesema advance ya asilimia 15 wameshalipa, na anatakiwa kuwa kashafanya mradi kwa zaidi ya asilimia 15 na kazi ionekane ndiyo araise tena certificate lakini mkandarasi bado hajafikisha hizo asilimia 15 yeye yupo kwenye asilimia 12.8. Mradi huo wanalipwa zaidi ya milioni 237 kwa mradi wa siku 270 na ameingia site mwezi wa 7, amelipwa 20/ 06/ 2023.
Leo tar 15 mwezi wa 6, 2024 bado 360 na huku mkandari mradi wake ni wa siku 270 hakuna hata dalili ya Bwawa wala tenki kujengwa na leo ni siku ya 360 nje ya ya muda siku 90 za siku za mradi, Waziri kasema anaona hata wakimpatia miaka mingine 20 bado hataweza kuukamilisha mradi huo ndio maana wameshabadilisha wakandarasi wa kutosha, hivyo amesema Mkandari wa aina yake kwenye Wizara ya maji nafasi hiyo haipo.
Waziri amesema kwa sababu hakuna maji chini ya Ardhi ndio sababu ya kujengwa kwa mabwawa hayo huko Monduli ili kutatua shida ya maji.