Naichukia ndoa yangu..

Naichukia ndoa yangu..

condorezaraisi

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2011
Posts
225
Reaction score
116
JF nimeolewa miaka nane iliyopita nikiwa na 21 years old,nimekaa na mme wangu katika ups and down za ndoa ..
Ila mme wangu naona ana mambo mengi ya ujana,dharau na kutojari familia , hakui najaribu kumwelewesha misingi ya ndoa na kumwelewesha pale anapoenda kinyume
lakini inakuwa kazi bure.
Kinachoniuma nadhani nampenda sana mme wangu akinikosea ninaumia hata week nzima siwezi kula ,kulala Napata shida wakati yeye
Anakuwa normal na hana hata muda wa kuomba msamaha.
Nahisi haya mapenzi niliyonayo kwa mme wangu yananiua ama kunipeleka vibaya.
Mtaalam mmoja aliniambia Tatizo langu nina 75% ya penzi kwa mme ,nijaribu kuweka 50/50%
Najitahidi kufanya hivo na ku-ignore yote anayoyafanya ,,mwisho wa siku nashindwa najikuta naendelea kuumia zaidi na kunyong’onyea .
Ni mengi anayonikosea.
JF ninawezaje kupunguza haya mapenzi ili niishi kwa Amani?
Nisaidie nakufa siku si zangu..nifundisheni nilipunguze vip hili penzi kwa baba chanja nisiumie

Mama Clea
 
lakini Boss mbona hujatoa anagalizo asije akaharibu mazima mwenzio?


Kupunguza ni kutafuta sehemu ya kuyaelekeza......

Unatafuta mtu mwenye extra kuzidi ya mumeo...game over....lol
 
Pole sana. Omba Mungu atakusaidia. Na inabidi uombe sana. Mungu sio sukari inayokolea mara moja, lakini atasikiliza kilio chako na kumbadilisha.
Epuka na tamaa ya "kulipiza kisasi" au kitu cha namna hiyo
 
Kupunguza ni kutafuta sehemu ya kuyaelekeza......

Unatafuta mtu mwenye extra kuzidi ya mumeo...game over....lol

Hivi mkuu ule mwongozo wetu hakuna version 2 kwa ajili ya watu kama mama Clea?
 
siku moja kaa naye,mwangalie machoni mtamkie 'nakupenda sana darling' ......hakikisha naye anakuangalia machoni
 
Nitafute kwa ushauri zaidi - hii inahitaji faragha kuweza kuchukua 25% ya mapenzi kutoka kwa mtu!
 
JF nimeolewa miaka nane iliyopita nikiwa na 21 years old,nimekaa na mme wangu katika ups and down za ndoa ..
Ila mme wangu naona ana mambo mengi ya ujana,dharau na kutojari familia , hakui najaribu kumwelewesha misingi ya ndoa na kumwelewesha pale anapoenda kinyume
lakini inakuwa kazi bure.
Kinachoniuma nadhani nampenda sana mme wangu akinikosea ninaumia hata week nzima siwezi kula ,kulala Napata shida wakati yeye
Anakuwa normal na hana hata muda wa kuomba msamaha.
Nahisi haya mapenzi niliyonayo kwa mme wangu yananiua ama kunipeleka vibaya.
Mtaalam mmoja aliniambia Tatizo langu nina 75% ya penzi kwa mme ,nijaribu kuweka 50/50%
Najitahidi kufanya hivo na ku-ignore yote anayoyafanya ,,mwisho wa siku nashindwa najikuta naendelea kuumia zaidi na kunyong'onyea .
Ni mengi anayonikosea.
JF ninawezaje kupunguza haya mapenzi ili niishi kwa Amani?
Nisaidie nakufa siku si zangu..nifundisheni nilipunguze vip hili penzi kwa baba chanja nisiumie

Mama Clea
Unajua dada yangu tatizo ulilo nalo wewe ndilo nililo nalo na mimi kwa mke wangu, Nadhani nikutafute tubadilishane uzoefu na tuangalie the way forward plz ni-PM tu-arrange.
 
Mumeo ana umri gani? Je ni muelewa?
 
Mwanaume hasa mumeo kumpenda peke yake haitoshi… inatakiwa pia kumuelewa, na ukisha muelewa kujua hasa jinsi gani ya kudeal na huyo mtu. Mie sikushauri usimuache for believe me you utaempata atakua hivo hivo otherwise uamue kua unataka kuishi peke yako which is not good (IMO). Na labda umuache kwamba its to the maximum and affecting you as a person.

The first step usha mjua nivipi yupo, I think inayofuata ni kua mkae chini for a hard discussion. (which I believe ushafanya ) saizi badilisha technique kwa kuonesha you no longer care or give a damn… Yes I know ni ngumu saana but for the sake of your marriage try. La msingi atimize wajibu wake, if you have plans za maendeleo mziweke katika ratiba then yale ambayo anafanya kwa wakati wake usimfuatilie kabisa…. Kuumia kwako ni sababu you CARE a lot… acha alone kwamba wampenda.

Unapomlaumu, unaposhindwa kula kwa ajili yake, unaporeact labda kwa kupunguza kufanya responsibilities dhidi yake; yoote haya anaone kabisa but kwa ujeuri aweza pretend hajanotice ili kut kukukomoa… WHY? My assumption kisha kuweka katika kundi la wanawake walalamishi mno (na believe me you 8 years of reasoning kwa upande wake yeye kaichukulia ni 8 years ya mwanamke mlalamishi – Belief inayomfanya hata uongee la maana asikusikilize kabisa)

Nakusihi jaribu kubadilika hisia za hasira na kujali saana matendo yake it may help hata waweza shangaa na in the long run itampa wasi… Usimpe kabisa hio nguvu yakusema aweza katisha maisha yako… Wanaume dear anakuzika siku hio hio analala na hawara (hasara to your loved ones na watoto) Hivo be strong… Hatoki mtu wala hateteleki mtu.

Naomba nikusifu saana kwa your 75% of energy katika ndoa… Mwanamke yeyote ambae ni a wife keeps her house in order with such energy… BEST OF LUCK

Pamoja Saana
AshaDii.
 
usidanganyike dia, tafuta wa kukuliwaza la sivyo utarun crazy, mwenzio yalinikuta tena makubwa kuliko yako, lakini once nilipata faraja mahala pengine mbona ndoa inadumu na ina zaidi ya miaka 12, go out there and find a someone, haitachukua muda kabla hujasahau shida zote.
 
Rudisha mkanda nyuma, uchunguze ni wapi ulipokosea. Inawezekana wakati wa uchaguzi ulirahisisha mambo. Huna ujanja, beba msalaba wako hadi mwisho.
 
Bibie upendo wakweli haujivungi mwaya

zaidi hapo muombee mumeo kwa Mungu aweze badilisha tabia yake

Wanaume wa sasa hivi spana mkononi ndugu

Unaweza sema uachane na huyu, utakutana na mwingine yupo mara 100 ya wa mwanzo,

vumilia bibie ila kuhusu vidumu usijaribu, utajiharibia mfumo wako wote wa maisha.
 
Mwaya tafuta hobbies, vitu vya kukushughulisha ambavyo vitakupa raha na excitement nyingi.

Ukishakuweza hilo ile attention ya saa zote itapungua na unaweza pata amani kidogo
 
  • Thanks
Reactions: Edo
Back
Top Bottom